Wednesday, September 26, 2012

Mwalimu amropokea Waziri

NAIBU Waziri wa Elimu na Ufundi Stadi, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi kwa muda Mwalimu wa Sekondari ya vipaji maalumu Ilboru, Potin Sumawe kwa madai ya kulewa kazini na kuropoka.

Majaliwa ambaye jana alilazimika kwenda shuleni hapo kuzungumza na wajumbe wa Bodi ya Shule, walimu na wanafunzi ili kufahamu kiini cha matatizo yaliyosababisha juzi wanafunzi kuandamana, alimsimamisha mwalimu huyo wakati kikao kikiendelea.

Wakati Naibu Waziri akihoji sababu za hali iliyoikumba shule, mwalimu huyo aliingilia kati na kuzungumza katika hali iliyosadikiwa kuwa ya ulevi akisema, “mkuu tupo hapa walimu, hawa wanafunzi wanaleta ugomvi sisi walimu tunafundisha”.

“Kwa nini unazungumza wakati hujapewa nafasi ya kuzungumza,” alihoji Majaliwa na kuamuru apelekwe hospitalini apimwe kubaini kama amechanganyikiwa au ni ulevi.

“Nimemwagiza Ofisa Utumishi kumpeleka hospitalini, kupimwa kama amechanganyikiwa na ripoti itakayotolewa iletwe kwangu, ili nijue ni ulevi au la; hivyo namsimamisha kazi na kuanza kupitia jalada lake, tuone kama anaweza kuonywa au la … tutachukua hatua,” alisema Majaliwa. Kutokana na tukio hilo, alionya watumishi dhidi ya unywaji pombe saa za kazi, huku akiwataka kuheshimu kazi kwa kufuata sheria ya utumishi wa umma.

“Kama mtumishi wa umma unavunja sheria kwa kunywa pombe kazini, utachukuliwa hatua, kwa kuwa hata yule mtoto uliyekabidhiwa kumfundisha, hutaweza kumfundisha kwa misingi mizuri, hivyo mfanye kazi kwa maadili,” alionya.

Alisema tabia ya ulevi kazini haikatazwi shuleni tu, bali sehemu yoyote mfanyakazi wa Serikali au sekta binafsi, haruhusiwi kufanya kazi huku amelewa, hivyo mtu akikutwa katika hali hiyo atafukuzwa kazi.

Baadhi ya walimu ambao hawakuwa tayari majina yao yaandikwe gazetini, walimwomba Naibu Waziri aifunge shule hiyo kwa muda, hadi wanafunzi watakapoandikiwa barua za kuitwa, kwa sababu walimu wamepoteza imani nao wakidai wanafunzi wanachochewa na viongozi wa juu serikalini, kuandamana.

Nao wanafunzi walimwomba Naibu Waziri, amhamishe Mkuu wa Shule, Jovinus Mutabuzi wakimtuhumu kwa ubadhirifu na kuwatishia wanapofuatilia taarifa za shule.

Mkuu wa Shule alisema kwa sasa hawezi kuongelea kitu chochote, kwa sababu bado yuko kwenye mazungumzo na Naibu Waziri na uamuzi wa kitakachoafikiwa utatolewa.

Juzi wanafunzi wa shule hiyo waliandamana hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishinikiza Mkuu wa Shule aondolewe.

CCM yajivua ‘gamba’

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, amesema katika kuhakikisha CCM inazidi kuwa na uhai na kupata ushindi katika uchaguzi mkuu mwaka 2015, Kamati Kuu ya Chama hicho imeamua kuwaengua wagombea wakongwe na kutoa nafasi kwa vijana.

Pamoja na hayo, habari za ndani za vikao vya chama hicho vinavyoendelea mjini hapa, zimebainisha kuwa Mwenyekiti huyo katika kuhakikisha mizizi ya ufisadi inakatwa ndani ya chama hicho, baadhi ya vigogo wakiwamo wabunge wagombea, majina yao yamekatwa huku wengine wenye majina makubwa wakipendekezwa kuendelea.

Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, mjini hapa jana jioni, Rais Kikwete alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, chama hicho kimebahatika kupata wagombea wengi wasomi na wengi wao wakiwa vijana jambo ambalo linatia matumaini.

“Jana (juzi) CC tulimaliza saa 6.30 usiku, kazi tuliyofanya ni kubwa na tumefurahi kwamba safari hii pamoja na kupata wagombea wengi wakiwamo wasomi, wengi ni vijana, kwenye Kamati hii tumeamua kuwapa nafasi zaidi vijana na wenzetu wakongwe wakapumzike,” alisema Rais Kikwete.

Alisema kati ya vijana wasomi waliojitokeza kuwania nafasi ndani ya chama hicho, wamo walio vyuoni jambo linalotia moyo kuwa bado CCM iko hai ambapo alibainisha wazi kuwa chama chochote cha siasa kikikosa mwamko wa vijana lazima kitakuwa na matatizo.

“Napenda nieleweke kuwa hatuwezi kuwa na chama cha watu wazima pekee, chama chenye mfumo huo hakitakuwa na mfumo mzuri wa uongozi, tumefanya hivi ikiwa ni fursa ya kukipa chama chetu uhai na taswira mpya lakini kubwa zaidi ushindi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015,” alisisitiza.

Alisema katika uchaguzi huo wa ndani wa chama, wanachokitarajia ni kupata timu ya viongozi wenye uadilifu, shupavu, hodari na wenye kukitetea chama, kwa maana nyingine alisisitiza kuwapo timu ya ushindi wa chama na si ushindi wa mtu.

“Na nasisitiza, hatutaki kiongozi mwenye ndimi mbili, maana nasikia kuna watu wanatishia eti wakikatwa huku kwenye ugombea wanakwenda vyama vingine, nasema hivi, wenye nia hiyo waende kwa sababu hadi kufikia kutishia hivyo ina maana tayari wana nafasi huko, tunawatakia kila la heri,” alisisitiza.

Aliwataka wagombea watakaoshindwa kwenye uchaguzi huo kutokata tamaa, kwa kuwa kushindwa kwao leo hakumaanishi hawawezi, bali ni kutokana na nafasi finyu lakini pia umuhimu wa mabadiliko na kutumia usemi kuwa kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi. “Hata Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere (Julius) alisema chama kwanza utu baadaye.”

Aidha, Mwenyekiti huyo alizungumzia suala la baadhi ya wagombea wa chama hicho kudaiwa kutoa rushwa hali ambayo inageuza uchaguzi huo kama biashara na kuwa wagombea wa namna hiyo hawafai kwa kuwa hawajiamini, wala kuthamini chama, bali uongozi na kuwahakikishia kuwa safari hii Takukuru haitakuwa mbali nao na wakikamatwa wasimlaumu.

“Sheria ya rushwa inaanzia kwenye chama, najua wapo watu ambao wanakifanya chama chetu kisemwe sana, nawaomba sana tutumie fursa hii kubadilika na kukipa chama chetu heshima,” alisema.

Kikwete alionya wagombea ambao wamesababisha uchaguzi wa CCM kugeuka vurugu za silaha na kuwatanabaishia kuwa wamekifedhehesha chama hicho.

“Watu mnafikia hatua ya kutumia mishale, bastola na mikuki, kugombea NEC tu mnashikiana silaha kweli? Jamani uchaguzi si vita.” Wakati NEC ikianza, Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama alisema idadi halisi ya wajumbe wa NEC ni 216 na waliohudhuria ni 196.

Tuesday, September 25, 2012

Wanajeshi: Wabadhirifu wapigwe risasi hadharani

Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba

HOJA ya adhabu kwa viongozi wanaotumia vibaya madaraka, ni miongoni mwa zilizotawala kwa Watanzania wengi wanaotoa maoni kwa ajili ya Katiba mpya, huku baadhi ya wanajeshi wakipendekeza kiongozi wa uraia anyongwe, mwanajeshi apigwe risasi hadharani.

Wanajeshi hao wametofautina na wananchi uraiani, ambao wengi wanapendekeza kiongozi anayefanya ubadhirifu, aondolewe mara moja, ashitakiwe kabla ya kustaafu au hata baada ya kustaafu na wengine wakapendekeza magereza maalumu ya viongozi.

Akitoa maoni mbele ya wajumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Mabadiliko ya Katiba katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 411KJ Ruhuwiko, askari Mwita Nyansango (26), alisema adhabu hizo zitarudisha uwajibikaji kwa viongozi.

Mbele ya viongozi wakuu wa kambi hiyo, ambao waliombwa waruhusu wapiganaji hao wawe huru wakati wa kujieleza, Nyansango alisema viongozi wa sasa hawafuati maadili, wanatumia vibaya rasilimali za wananchi kwa kuwa Katiba iliyopo, haijaweka wazi namna ya kuwawajibisha.

“Katiba ijayo iweke wazi, kuwa kiongozi anayepewa dhamana ya kuongoza jamii, ikiwa ni waziri kafanya ubadhirifu, napendekeza anyongwe ili iwe fundisho, akija mwingine ajue kuna kitanzi, kwa sisi wanajeshi, apigwe risasi.

“Tunasikia mambo ya Dowans na Richmond na tunachukia kusikia yanaendelea, halafu wahusika wanapewa nafasi ya kujitetea na wakifika mahakamani, wanapigwa faini,” alisema Nyansango ambaye ana elimu ya darasa la saba.

Nyansango pia alisema askari wa JWTZ, Polisi, Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), hawapaswi kuitwa wanajeshi kwa kuwa majeshi ya ulinzi ni ya nchi kavu, anga na majini.

Hoja hiyo ilifafanuliwa na Luteni Hassan Tagalile, ambaye ana Shahada ya kwanza, aliyetaka Katiba ijayo ifafanue kati ya JWTZ, Polisi, Magereza na JKT, ni chombo kipi ni jeshi la ulinzi na kipi chombo cha usalama.

Sajini Amedius Haule (51), ambaye ni Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Songea Mjini, alipendekeza askari wa ngazi za chini ya koplo, wawe na mwakilishi bungeni, kwa madai kuwa wao ndio wanaokutana na machungu ya Jeshi.

Koplo Abeli Mtanzamo (29), alipendekeza mawaziri wasitokane na wabunge, kwa madai kuwa akiwa waziri anafanya ubadhirifu akijua atajiuzulu uwaziri na kubaki na ubunge.

Koplo Elina Mwakitinga mwenye Diploma ya Ualimu, alipendekeza sheria za Jeshi zitambuliwe na Katiba na wanaotunga wajulikane hadhi zao kielimu na kuongeza kuwa ana wasiwasi sheria za Jeshi kwa sasa si shirikishi na zimerithiwa tangu ukoloni na kutengeneza watawala na watumwa jeshini.

Naye Koplo Shaban Mrope (33), alisema Tanzania ina madini mengi, lakini viongozi wameingia mikataba ya miaka mingi na kusababisha hata mtoto atakayemzaa, asifaidike.

Alisema nchi ina maliasili nyingi na ilipaswa kutoa elimu na afya bure na kama Serikali imeshindwa kufuta mikataba hiyo na kuweka ya muda mfupi, ipishe Jeshi kwa muda lifute mikataba hiyo.

Hoja hizo zilizotolewa jeshini, zilitolewa pia katika mikutano uraiani, ambako adhabu zilizopendekezwa zilikuwa tofauti. Kuhusu adhabu kwa viongozi wabadhirifu, mkazi wa kata ya Ruhuwiko, Songea Mjini, Anthony Leonard (26), alitaka Rais asiteue Jaji ili apate uhuru wa kutoa hukumu.

Alipendekeza kuwapo magereza ya viongozi na kuhoji; “kwa nini hakuna kiongozi aliye gerezani? Au wao hawaharibu?” Kijana huyo alisema kama rasimu ya Katiba mpya itakuja na kipengele ambacho taasisi ya urais inaruhusiwa kuteua Jaji, hatapiga kura na kama kutopiga kura ni kosa, yuko tayari kwenda jela.

Mkazi mwingine wa kata hiyo, Pascal Ndunguru (64), aliyependekeza mbunge asiwe waziri, alimhoji kiongozi wa wajumbe hao wa Tume, Profesa Mwesiga Baregu aeleze kwa nini amekuja kusikiliza wananchi bila kufuatana na mbunge wao.

“Profesa, wewe umefika hapa, yuko wapi mbunge wetu? Tunasikia ni waziri na hicho ndicho hatutaki kusikia, mbunge asiwe waziri atutumikie wananchi,” alisisitiza.

Simon Haule (80), mwenye elimu ya darasa la nne, alipendekeza Rais akitoka madarakani asipewe mshahara hadi kufa, bali alipwe pensheni kama mstaafu katika utumishi wa umma.

Monday, September 24, 2012

Polisi wamuokoa Askofu kanisani

MGOGORO uliolikumba Kanisa la Watakatifu Wote la Anglikana mjini Sumbawanga na kudumu kwa zaidi ya miaka mitatu, haujapata ufumbuzi wa kudumu baada ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo la Anglikana Tanzania,a Dk Valentino Mokiwa kujikuta katika wakati mgumu jana baada ya kunusurika kupata kipigo katika vurugu zilizoibuka kanisani.

Vurugu ziliibuka baada ya kusomwa tamko lililothibitisha kuwa nyumba ya maaskofu inamtambua Askofu Mathias Kasagara kuwa ni kiongozi wao halali wa kanisa la Anglikana la Watakatifu Wote Jimbo la Ziwa Rukwa mjini Sumbawanga.

Katibu Mkuu wa Anglikana, Dk Dickson Chilongani ndiye aliyesoma tamko hilo mara baada ya kumalizika kwa ibada iliyoongozwa na Dk Mokiwa. Dk Chilongani alisema Kasagara ni askofu wao halali kwa kuwa sehemu ya hoja za msingi za kamati ya usimamizi wa kanisa hilo zilidai kuwa uchaguzi uliomweka madarakani Askofu Kasagara uligubikwa na rushwa, si za kweli na nyumba ya maaskofu imeshindwa kuthibitisha.

Baada ya kauli hizo waumini walianza kupiga kelele ya kupinga maelezo hayo, hali iliyosababisha mjumbe wa Kamati ya kusimamia kanisa hilo, Fulgence Lusunzu kushika kinasa sauti na kueleza kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuwa rushwa ilitumika kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi huo uliofanyika zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Alisema uamuzi wa nyumba ya maaskofu haukuwapa fursa ya kusikiliza upande wa walalamikaji, ilihali ushahidi upo wazi, kutokana kauli hiyo zilianza fujo zilizosababisha Askofu Mokiwa kutolewa lugha chafu, kuvuliwa kofia yake ya kiaskofu, huku wengine wakirusha viti ambavyo alivikwepa hadi alipoondolewa akiwa chini ya polisi waliokuwa wamevalia kiraia.

Pamoja na kuondolewa kwa Askofu Mokiwa, kanisa hilo liliendelea kuwa uwanja wa vita huku waumini wakisikika wakidai kuwa ni heri kanisa hilo lifungwe kuliko Askofu Kasagara kuliongoza.

Awali tangu asubuhi, polisi waliovaa kiraia walitanda katika viunga vya kanisa hilo ambapo Askofu Mokiwa aliwasili na kulakiwa vizuri na waumini wake waliokuwa wakishangilia kwa nyimbo.

Hata hivyo, tayari waumini wa kanisa hilo walionya kwamba Askofu Kasagara asikanyage kwenye eneo hilo, kwani kufanya hivyo kungehatarisha amani, onyo ambalo upande wa Askofu Kasagara walitii hivyo askofu huyo mwenye makazi yake wilayani Mpanda alibaki katika nyumba moja ya kulala wageni alikokuwa amefikia.

Mmoja wa waumini, Julius Michael alisema kwa kuwa waumini wa Jimbo la Rukwa hawamtaki Askofu Kasagara, hakuna sababu ya kuwalazimisha isipokuwa nyumba ya maaskofu inapaswa kuangalia uwezekano wa kuligawa jimbo hilo.

Alisema Serikali imegawa mkoa wa Rukwa na kuzaa Katavi, na kwamba hakuna umuhimu wa kuwalazimisha waumini kumpokea mtu wasiyemtaka.

Mgogoro katika kanisa hilo umedumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa, ambapo siku za nyuma waumini hao walimzuia Askofu Mkuu Dk Valentino Mokiwa kumsimika Askofu huyo na badala yake alisimikwa Juni 16 mwaka jana, mjini Mpanda.

Kutokana na mgogoro huo, ilifunguliwa kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sumbawanga na waumini wa Anglikana wakiongozwa na Fulgence Rusunzu na Rojas Bendera na wenzao 191 yenye namba 11/2011 wakipinga kuchaguliwa kwa askofu Kasagara kuwa kiongozi wa Dayosisi hiyo. Kesi hiyo iliondolewa baada ya pande mbili zinazovutana kukubaliana kuwa baraza la maaskofu ndilo lenye dhamana ya kutatua mgogoro huo.

Kinana ang'atuka CCM

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Abraham Kinana, amesema hatogombea tena nafasi za vikao vya juu kwa kuwa muda wa miaka 25 aliyotumikia katika nafasi hizo unatosha.

Kinana aliyasema hayo mjini Dodoma wakati akizungumza na gazeti hili na kubainisha kuwa anaamini kitendo cha kung’atuka kwake ni kizuri na kitatoa nafasi kwa wanaCCM wengine wazuri nao watoe mchango wao kwa chama hicho.

“Sijagombea kwa kuwa miaka 25 ya kushiriki katika vikao vya juu inatosha na ni vizuri kung’atuka, naamini kuna wana CCM wengi wenye sifa na uwezo wa kuongoza chama,” alisema Kinana.

Alisema suala la uongozi ni la kupokezana vijiti hivyo kwa sasa ni wakati wake kukabidhi vijiti alivyo navyo kwa wengine. Wakati Kinana akitoa kauli hiyo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alimsifu Kinana kwa uamuzi huo na kuuita kuwa ni uzalendo.

“Tunashukuru kwa uzalendo, ujuzi na uzoefu alioonesha katika kipindi chote alichoshika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama, hata hivyo, napenda nisisitize kutokana na sifa alizonazo bado chama chetu kinamhitaji,” alisema Nnauye.

Alisema kung’atuka kwake kuwania nafasi za vikao vya juu ndani ya chama hicho hakumaanishi kuwa chama hicho hakitoendelea kumtumia pale kitakapomhitaji, kwa kuwa uzoefu wake na utendaji wake ni mtaji ndani ya chama.

Alisema pamoja na kuamua kuachia ngazi, Kinana anaendelea kushika nyadhifa nyingine ndani ya chama hicho, ikiwamo ya Uenyekiti wa Bodi ya vyombo vya habari vya CCM vya Uhuru na Mzalendo.

Wakati huo huo, Nape amesema wagombea wa CCM wanaolalamika nje ya vikao na kutoa vitisho iwapo hawatapitishwa na vikao vya chama hicho, wanajiharibia sifa na kuonesha wazi kuwa hawawezi kuhimili vishindo vya uchaguzi.

Aidha, amesema mchujo wa wagombea nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaweza kuchukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kutokana na idadi kubwa ya wagombea waliojitokeza kuwania nafasi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema hawatashughulikia malalamiko na vitisho vya wagombea yanayotolewa barabarani.

“Kama wanataka wafikishe malalamiko yao kwenye vikao halali tutashughulikia, lakini wakilalamika au kutoa vitisho inaonesha wazi uwezo wao wa kuhimili pressure ni mdogo, hasa ikizingatiwa kuwa siasa za sasa zimejaa pressure,” alisema Nnauye.

Alisema mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu nani apite na nani asipite ni vikao vya chama ambavyo ni Kamati ya Maadili, CC na NEC.

Hivi karibuni, Mbunge wa Musoma Vijijini, ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nimrod Mkono, alikaririwa na vyombo vya habari akisema kama jina lake halitarejeshwa katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Taifa, atahakikisha inaeleweka.

Pia mbunge wa Kahama, James Lembeli aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari akisisitiza kwamba hatokubali kuenguliwa katika uchaguzi huo kwa visingizio vya misimamo yake bungeni.

Aidha, Nnauye aliweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna mgombea yeyote aliyeenguliwa na vikao vya chama hicho na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni kwa kamati ya maadili kupitia majina na kutoa mapendekezo yatakayopitiwa na CC na uamuzi wa mwisho ya kuenguliwa mgombea utafanywa na NEC.

“Kazi ni kubwa kinachofanyika ni Kamati hii ya Maadili kupitia jina moja moja la kila mgombea na kisha kuwapatia alama ya A, B, C, D na E lakini katika vikao vingine alama hizo zinaweza kubadilika kulingana na vikao hivyo,” alisema.

Wednesday, September 19, 2012

Mkorogo wasababisha hedhi kukoma

Mkufunzi wa masuala ya Uzazi wa Mpango kutoka kampuni ya T-Marc, Grace Dibibi akielekeza jambo kuhusu njia bora za uzazi wa mpango kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), (hawapo pichani) katika ofisi zao zilizopo eneo la Tazara, Dar es Salaam jana.

WANAWAKE nchini wamehadharishwa juu ya matumizi ya dawa za kujichubua, kwani husababisha madhara yakiwamo ya kukoma kwa hedhi kabla ya umri.

Dawa hizo za mkorogo, zinaweza kusababisha kukoma hedhi kwa mwanamke mwenye umri wa hata miaka 30 hadi 35, tofauti na kawaida ya miaka 45.

Hayo yalibainishwa jana na mkufunzi wa taasisi isiyo ya Serikali ya T- MARC, Grace Dibibi alipowasilisha mada kuhusu Uzazi wa Mpango kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dar es Salaam jana.

Pia alihadharisha wanawake juu ya tabia ya kusafishwa vizazi mara kwa mara, kwani nayo husababisha kutojijenga ukuta ndani ya viungo vya uzazi na hivyo kushindwa kushika ujauzito.

Dibibi alisema wanawake wanatakiwa kuwa makini ili kupanga uzazi na kuzaa kwa muda wanaotaka, huku akisisitiza kuwa dawa za uzazi wa mpango ni salama, bali zenye vichocheo zinazoweza kusababisha madhara kwa baadhi ya wanawake.

Kuhusu suala la wanawake kuchelewa kuzaa baada ya kutumia njia za uzazi wa mpango, alishauri kuonana na madaktari wanawake na kuwaelezea historia ya familia kabla ya kutumia njia hizo.

“Kuna watu kwenye familia huzaa mtoto mmoja, lakini wanapozaa tu huanza njia za uzazi wa mpango bila ushauri wa wataalamu,” alieleza mkufunzi huyo.

Alisema njia hizo zote za uzazi wa mpango, hutumiwa isipokuwa ya kufunga uzazi, kwani takwimu zilizopo zinaonesha kuwa ni wanaume watatu tu nchini ndio walifungwa uzazi na wote wanatamani kurudishiwa.

Alisema kwa wanawake ni asilimia 20 ndio waliofunga, hasa wasomi, lakini akasema hajui sababu ya wasomi kupenda njia hiyo.

Mhamasishaji wa taasisi hiyo, Shani Pius alisema wanawake wengi hawapendi kutumia kondomu za kike kwa madai kuwa zina hatua nyingi za kufuata wakati wa kuzivaa kutokana na umbo lake, jambo ambalo linakera wapenzi wao.

Alisema mara nyingi kondomu hizo hutumiwa na wanawake wanaofanya biashara ya mapenzi ili kujikinga pale wanaume wanapokuwa wabishi, lakini si kwa wapenzi wa kawaida.

Tuesday, September 18, 2012

Found at Beemp3.com

Tapeli la Kijerumani latikisa Dar

• Awaliza Watanzania mamilioni

MTU mmoja raia wa Ujerumani, amewaliza Watanzania wengi baada ya kufanikiwa kuiba kwa njia za kitapeli mamilioni ya fedha.

Raia huyo ambaye amekuwa akibadilisha majina, kwa zaidi ya miezi miwili sasa, amejichimbia katika hoteli kubwa za kitalii akijifanya kuwa wakala wa dawa za mifugo na wanyama kwa kushirikiana na watu wengine watatu raia wa Tanzania.

Habari za kuaminika zilizothibitishwa na askari polisi jijini Dar es Salaam, zimesema mjerumani huyo anayekisiwa kuwa na umri kati ya miaka 65 na 70, amekuwa akitumia jina la kampuni moja kubwa ya dawa za mifugo (jina linahifadhiwa) ya hapa nchini kufanikiwa utapeli huo.

Mmoja wa watu waliotapeliwa, Martin Peter, alisema wiki iliyopita, mjerumani huyo pamoja na Watanzania watatu, walifanikiwa kumtapeli jumla ya shs milioni 25, kwa ahadi ya kumpa zabuni ya kuuza dawa za mifugo katika mkoa wa Katavi.

Akisimulia kwa undani alivyotapeliwa, Mariselina alisema: “Jumanne wiki iliyopita, nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Martin ambaye alisema tulisoma naye sekondari zaidi ya miaka 10 iliyopita.

“Ingawa sauti sikuwa naikumbuka, lakini baada ya kujieleza, nilikumbuka kwamba ni kweli nilisoma na mvulana huyo na alikuwa rafiki yangu.”

Mariselina alisema kuwa ‘rafiki’ yake huyo, alimwambia kuwa kwa sasa yuko mkoani Katavi katika shirika la hifadhi ya taifa, na kwamba alikuwa akihitaji amsaidie kupata dawa za wanyama kwa kuwa kulikuwa na mlipuko wa ugonjwa katika hifadhi hizo.

“Aliniambia kuwa anahitaji nimsaidie kwenda katika kampuni ya (anaitaja) na kuonana na (anamtaja) ambaye anasema kuwa huwauzia dawa hizo kila wakati.

“Alisema safari hii hataki kununua kwake, kwa vile amekuwa hampi cha juu (bakshishi), na kwa sasa ameona anitafute mimi ambaye niliwahi kumsaidia tukiwa shuleni ili nami nipate faida kidogo,” alisema.

Mariselina aliendelea kudai kuwa, Martin alimpa namba ya mtu huyo wa kampuni ya dawa, na kwamba akiisha inunua, aende hadi katika hoteli ya kitalii ya (anaitaja) ambako atamkuta mkuu wake wa kazi, ambaye ni raia wa ujerumani ambaye atanunua dawa hizo.

Mama huyo amedai, awali aliingiwa na hofu, lakini akapata nguvu baada ya kupiga simu na mtu wa kampuni ya dawa aliyekubali kumuuzia dawa.

“Martin pia alinipa namba za huyo mzungu na kuniambia nijifanye ninazo dawa zakuwauzia na nilipopiga kweli alinipokea na kuniambia niende hotelini.

“Kule walinihoji kwa ukali kama kweli nitawaletea dawa halisi, huku akidai kuwa anaogopa sifa mbaya za utapeli kutoka kwa Watanzania,” alisema na kuongeza;

“Yule mzungu alionekana mwenye fedha nyingi, kwani nilikuta ‘briefcase’ ndogo ikiwa imejaa dola, na akanitaka nipige picha yangu, na kisha nimletee kwanza sampuli mbili za dawa zenyewe”

Anasema hata baada ya kukamilisha, aliwasiliana na yule mtu wa kampuni ya dawa ambaye alimwambia kuwa hawezi kumuuzia dawa kidogo, badala yake kama anataka anunue nusu ya mzigo uliotakiwa ambao ni shs milioni 40.

Mwanamke huyo anasema, wakati akisita, alipigiwa simu na mjerumani huyo, na kumwambia kuwa aachane na sampuli na kama hana uwezo wa kuleta mzigo wote, ajitahidi kuletea nusu kwani ulikuwa unatakiwa haraka siku hiyo hiyo.

“ Martin naye alinihimiza kama kweli bosi wake yule mzungu kaniambia nimpelekee, basi nifanye hivyo haraka na kwamba tutagawana faida nusu kwa nusu.

“Anilinipa hadi namba ya akaunti ya benki, ili nikiishalipwa, nimwekea fedha zake,” alisema.

Hata hivyo, Mariselina anasema, walikubaliana na mtu wa kampuni ya dawa kukutana Mlimani City akiwa na fedha na wakakamilisha ununuzi huo.

“Kwanza nilipoona dawa hizo, nilimpigia Martin na kumsomea maandishi yake na namna zilivyofungwa na akakubali kuwa ndizo zenyewe, hivyo nifanye haraka kununua na kuzipeleka kwa mzungu kabla ya saa tisa alasiri.

“Ajabu, nilipofika katika hoteli ile na kupiga namba ya mzungu kumtaarifu kuwa nimefika, simu ilikuwa imezimwa. Nikampigia Martin, nae yake ilikuwa kimya, na hata nilipopiga kwa yule mtu wa kampuni ya dawa, nayo ilikuwa imezimwa,” anasema.

Mariselina anasema, alijaribu kuuliza wafanyakazi wa hoteli ile, ambao walishindwa kutambua kuwepo kwa mgeni mjerumani mahali hapo.

Mwanamke huyo anasema hisia za kuibiwa ziliingia akilini, na kulazimika kukimbilia polisi.

“Jambo la kushangaza, nilipowaambia pale Central, askari waliyekuwapo walicheka na kuniambia, mama umeibiwa ndio mchezo wa huyo mzungu na kwamba ameshawaibia watu wengi kwa mtindo huo.”

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova hakuweza kupatikana baada ya simu yake kuita muda mwingi bila kupokelewa.

Hata hivyo, ofisa mmoja wa polisi aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema mjerumani huyo anasakwa kwa matukio hayo, akishirikiana na Watanzania wengine watatu.

“Amewaliza wengi. Anawatumia watu watatu ambao karibuni tutawatia mikononi,” alisema.

Wengine watumia SMS

Katika hatua isiyoeleweka, watu wasiojulikana wamekuwa wakiwatumia watu mbalimbali jijini Dar es Salaam, jumbe zenye kuwataka kuwasiliana nao kwa madai ya kufanya biashara nao.

Watu hao ambao wanadai kuwa na makazi maeneo ya Sinza, lakini bila kuonesha wanamiliki kampuni gani mara kadhaa wameingilia namba za watu na kuwaomba kuwasiliana nao na kufika katika eneo hilo ili kufanya biashara ambazo hazitajwi.

Moja ya jumbe zinazotumwa kwa watu zinasema kupitia namba 0653634042 na 0767945946; ‘ Habari, …(wanataja jina lako) kampuni yetu imepata namba yako kuwa unaweza kufanya kazi nasi kwa muda wako wa ziada. Kwa maelezo zaidi, wasiliana kwa namba 0653634042 au 0716334595.

Hata hivyo, mmoja wa watu waliowahi kutumiwa ujumbe huo, Violeth Bago wiki iliyopita akiandamana na watu wengine wawili, kweli alikoelekezwa, lakini katika namna ya kushangaza, watu hao walidai kuwa amechelewa kufika, hivyo afike tena kesho yake saa 5 asubuhi kwa majadiliano.

Hata hivyo, watu hao hawasemi ni kampuni gani na inahusiana na biashara gani, hali inayotia mashaka ya uhalali wao

Wednesday, September 12, 2012

mwanamke ajifungua farasi

September 11 ni siku ambayo kwa Marekani ni alama kubwa kutokana na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa miaka 11 iliyopita, lakini september 11 2012 imekua alama kwa Nigeria baada ya mwanamke kujifungua mtoto wa farasi.

Tukio limetokea wakati mwanamke huyu akiwa kanisani kwenye maombi huko Sapele-Benin Expressway Edo state ambapo alijifungua wakati wakiwa kwenye maombi.

Mtandao wa Naijagists umeripoti kwamba mwanamke huyu kabla ya kujifungua alipiga sana kelele kama yuko kwenye chumba cha kujifungulia wakati maombi yakiendelea ambapo damu zilianza kumtoka sehemu zake za siri na baadae kujifungua huyu mtoto wa farasi ambae alifariki kabla ya waandishi wa habari kufika kwenye hilo kanisa.

Mtumishi wa Mungu aliepata nafasi ya kuzungumza baada ya hii ishu kutokea amesema wamekua wakishuhudia miujiza mingi ikifanyika kanisani kwao lakini hili la mwanamke kujifungua mtoto wa farasi ndio limetokea kwa mara ya kwanza.

‘Walimu wanaopewa mimba na wanafunzi washitakiwe’

BAADHI ya wanafunzi wa sekondari wilayani Mpanda na Mlele mkoani Katavi wamejitokeza mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kupendekeza Katiba ijayo ibane walimu wa kike ambao wanapewa ujauzito na wanafunzi wao.

Pia wanafunzi hao walipendekeza wanafunzi wanapopeana mimba, mvulana na msichana, wote wachukuliwe hatua za kisheria kwa kushitakiwa na si msichana kufukuzwa shule tu wakati mvulana anashitakiwa na baadaye kufungwa.

Wanafunzi hao pia walipendekeza mabadiliko ya mitaala ili kumpunguzia masomo mwanafunzi wa sekondari na wakapendekeza lugha ya Kiswahili iwe ya kufundishia kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne.

Sabath Katabi ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Sekondari ya Kasokola wilayani Mulele, alisema maisha ya shule yana wanafunzi na walimu na mwalimu wa kiume anapompa mimba mwanafunzi wake, anafukuzwa shule na kushitakiwa.

“Naomba Katiba mpya pia iseme kuwa mwalimu wa kike anayepewa mimba na mwanafunzi wake pia afukuzwe kazi na ashitakiwe, kwani naye atakuwa amefanya kosa kufanya mapenzi na mwanafunzi wake,” alisema Katabi.

Mwanafunzi huyo alisema hajawahi kuona walimu wa kike wanaofanya mapenzi na wanafunzi wao wakichuliwa hatua, jambo ambalo alisema ni ubaguzi mkubwa wa kisheria kwa kuwaonea walimu wanaume ambao wanajikuta kwenye uhusiano na wanafunzi wao, kwa sababu ya kujaribiwa na wanafunzi hao.

Mikisedeki Nyambwago ambaye ni mwanafunzi wa Sekondari ya Milala alitaka wanafunzi wa kike ambao wanapachikwa mimba na wanafunzi wavulana nao wachukuliwe hatua za kisheria, kwa kushitakiwa ili wawe waoga wa kufanya mapenzi wakiwa shuleni.

“Sheria inabagua, mvulana akifanya mapenzi na msichana, mvulana anafukuzwa shule na kushitakiwa, lakini msichana anafukuzwa shule na hashitakiwi, kwa nini wakati wote hawa wamefanya kosa la jinai?”

Alihoji mwanafunzi huyo. Nasri Lubeba mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Sekondari Milala, alipendekeza Katiba itamke kuwa mwanafunzi wa kike anayepata ujauzito, akishajifungua apewe fursa ya kurudi shuleni ili aendelee na masomo.

Alipoulizwa na Dk Sengondo Mvungi kama haoni kuwa hiyo itachochea wanafunzi wengi kupata ujauzito, Nasri alisema haiwezekani, kwani ujauzito unatokea kwa bahati mbaya na hakuna mwanafunzi anayedhamiria kupata ujauzito akiwa shuleni.

“Ile inatokea kwa bahati mbaya, sidhani kama kuwapo kwa sheria hiyo kutachochea ngono shuleni, ila kutampunguzia mzigo msichana, kwani maisha yake asiporudi shule yanakuwa mabaya zaidi,” alisema msichana huyo.

Pia alipendekeza wanafunzi wanapopeana mimba iangaliwe adhabu ambayo haitawakandamiza au kuumiza kichanga kinachozaliwa, bali itafutwe namna ya kuwasaidia ili waendesha maisha yao ya baadaye. Kwa upande wake, Marko Bwire alipendekeza Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia hadi kidato cha nne kwa maelezo kuwa wanafunzi wengi wanafeli mitihani ya kidato cha nne kutokana na kutoielewa vizuri lugha wanayofundishiwa.

“Unakuta mwanafunzi shule ya msingi alikuwa anafanya vizuri, akienda sekondari kwa vile huko masomo yote yanafundishwa kwa Kiingereza, lugha inakuwa kikwazo na kusababisha afeli,” alisema Bwire.

Flora Kashindye wa kidato cha pili Shule ya Milala, alipendekeza Katiba iilazimishe Serikali kujenga maabara kwenye sekondari za kata, ili kupunguza idadi ya wanafunzi wanaofeli.

Alisema wanafunzi wanaosoma shule za kata hawafanyi mitihani ya vitendo, bali wanafanya ya nadharia tu hali inayosababisha washindwe kuhimili ushindani na shule zingine.

Mwanafunzi mwingine, Peter Kalindi yeye alitaka mitaala iboreshwe na isibadilishwe mara kwa mara, kwani kufanya hivyo kumechangia kuvuruga elimu nchini, wakati Basori Masunga akipendekeza Serikali iweke viwango vya ada kwa shule binafsi ili hata wazazi wenye kipato kidogo wasomeshe watoto wao.

Waandishi wa habari waandamana kulaani mauaji ya mwenzao

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi amepongeza waandishi wa habari walioandama jana Dar es Salaam kwa kuzingatia sheria.

Dk Nchimbi ambaye ‘alivamia’ Viwanja vya Jangwani jana ambako maandamano hayo ya kulaani mauaji ya mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi yaliishia, alisema waandishi hao walifuata utaratibu.

“Hivi ndivyo inavyotakiwa, kufuata sheria, kwani walitoa taarifa Polisi lakini hata walipoambiwa kwamba Mnazi Mmoja njia ni nyembamba hivyo wahamie Jangwani hawakusita na walifanya hivyo.

“Ni tofauti na watu wengine ambao wakiambiwa msipite huku hali hairuhusu hulazimisha na matokeo yake ni mtafaruku na Jeshi la Polisi,” alisema Nchimbi alipozungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Jangwani. Alitoa mwito kwa makamanda wa Polisi wa mikoa kukaa na wanahabari na kujadiliana ili wafanye kazi pamoja na kuondokana na migogoro ambayo haina ulazima.

Waziri Nchimbi ambaye alipata kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, alisema yote yaliyozungumzwa na wanahabari jana Jangwani kwa Serikali yatafanyiwa kazi bila kusita.

Wahariri na waandishi wa habari wakiwamo waliopata kufanya kazi katika vyombo vya habari, waliandamana kimyakimya kulaani mauaji ya Mwangosi yaliyotokea Iringa katika maandamano ya Chadema, siku 10 zilizopita.

Mwangosi ni mwandishi wa kwanza nchini kuuawa akiwa kazini na wa 38 mwaka huu na kufikisha idadi ya waandishi 46 waliouawa wakiwa kazini duniani kote.

Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, Waziri Nchimbi ambaye awali alilakiwa na uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na kupanda jukwaani alijikuta akizomewa na kutakiwa kuondoka eneo hilo.

Awali akiwa peke yake, baada ya kuegesha gari mbali na eneo la mkutano, Nchimbi alitembea hadi walikokuwa wanahabari hao na kupokewa kabla ya kukumbana na kadhia hiyo.

Waandishi wa habari walipoulizwa ni wangapi wanataka Waziri ahutubie, walikataa na kumtaka aondoke huku wakihoji alichofuata.

Lakini tofauti na Nchimbi, aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayeaminika kuwa kada na mwumini wa Chadema, Dk Azaveri Lwaitama, bila kualikwa alipewa fursa ya kuhutubia mkutano huo.

Maandamano hayo yalianzia Channel Ten na kuishia Jangwani huku washiriki wakiwa na mabango ya kulaani mauaji hayo na wengine wakiwa na mfano wa silaha na baadhi yao wanaoaminika ni waandishi wa Kampuni ya HaliHalisi inayochapisha magazeti ya MwanaHalisi (lililofungiwa) na Mseto, walionekana na mabango yakilaani kufungiwa kwa gazeti hilo.

Akizungumza katika Viwanja vya Jangwani, Katibu Mkuu wa TEF, Neville Meena alisema mauaji ya Mwangosi yanaonesha kuwa mazingira ya kufanyia kazi kwa wanahabari si salama.

Alisema wahariri na waandishi wa habari walikuwa na uwezo wa kufanya jambo kubwa kupitia kalamu na kamera zao zaidi ya maandamano, lakini waliamua kutumia njia ambayo wananchi wa kawaida wanaitumia kudai haki zao.

Alisema TEF ilianza kwa kutoa tamko la kulaani na kuunda tume ya watu watatu ambayo itafanya utafiti wa kihabari kuhusu tukio hilo, utakaotumika kupata maazimio ya wadau wa habari.

Tume hiyo imeundwa na mjumbe kutoka TEF, Baraza la Habari Tanzania (MCT) na kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini. Meena alitaka waandishi wa habari kuendelea kuhabarisha wananchi kwa kufuata misingi ya taaluma ya habari.

“Tuendelee kufanya kazi, bila vyombo vya habari hakuna kitu kitakachoendelea na ndiyo maana hata Rais akitaka kuhutubia wananchi kila mwezi haendi Jangwani bali anatumia vyombo vya habari kufikia Watanzania zaidi ya milioni 40.”

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC), Jane Mihanji pamoja na kulaani mauaji hayo kwa nguvu zote, alitaka Polisi kutambua kuwa mwandishi anapokuwa kazini anatakiwa kuheshimiwa kwa kazi yake kama inavyofanywa kwa polisi akiwa kwenye sare. Mhariri Mtendaji wa Nipashe, Jesse Kwayu alisema:

“Kama Mwangosi angekufa kwa njia nyingine, kingekuwa kifo cha Mungu, lakini kwa kuwa ameuawa kikatili ndiyo maana tuko hapa.

“Damu yake ndiyo mwanzo wa kubadilisha mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini, wajue kuwa kodi za wananchi kama sisi ndizo zinazolipa mishahara, kuwanunulia magwanda kwa kazi ya kulinda raia na si kuua.”

Dk Lwaitama aliyetambulishwa kama rafiki wa wanahabari, alitaka waandishi kutochukia polisi wa ngazi ya chini na badala yake wachukie wanasiasa wanaowatuma na kuwatumbukiza katika siasa. Mwakilishi wa Africa Media Group, Dina Chahali alishukuru wanahabari kwa umoja wao wa kulaani mauaji ya Mwangosi na kuwa huo ndio mwanzo wa kudai haki ya habari na wanahabari.

Meena alipoulizwa baadaye na gazeti hili iweje Dk Nchimbi azuiwe kushiriki na Dk Lwaitama aruhusiwe, alisema hakuna aliyealikwa kwenye maandamano hayo zaidi ya waandishi wa habari na Dk Lwaitama alikuja kama wananchi wengine walivyojitokeza.

“Dk Lwaitama hakupata mwaliko, ila penye watu wengi panakuwa na mengi kama unavyojua ... sisi wenyewe tunashangaa, ni kupitiwa tu ila naye hakupewa mwaliko,” alisema bila kufafanua kama wananchi wengine nao walikuwa na haki ya kupanda jukwaani kuhutubia wanahabari.

Arusha Mkoani Arusha, polisi walifika eneo la Jengo la CCM la Mkoa, kuzuia maandamano ya waandishi waliokuwa wamejikusanya wakiwa na mabango yao, yenye ujumbe mbalimbali wa kulaani mauaji ya Mwangosi.

Polisi walieleza kuwa wanakabiliwa na uhaba wa askari wa kulinda maandamano hayo, kwa sababu ya ugeni mkubwa wa Mkutano wa Mazingira. Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), Eliya Mbonea aliwaomba waandishi kutii amri ya Polisi, huku akiwasomea taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Lotson Mponjoli ya kuzuia maandamano hayo.

Tuesday, September 11, 2012

Chadema wamsusa Tendwa, wamtisha

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kusitisha kufanya kazi na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa na kumtishia kikisema kama ana wendawazimu, ajaribu kukifuta aone moto wake.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akitoa uamuzi wa Kamati Kuu ya Chama hicho iliyokutana juzi kujadili masuala mbalimbali ya kisiasa nchini.

Mbowe alisema yuko tayari kuchukua maelekezo ya karani kuliko ya Msajili na kwamba hawatapokea maelekezo yake wala kumheshimu hadi atakapoondolewa katika nafasi hiyo na kuteuliwa mwingine.

“Hatutahudhuria kikao chochote cha Tendwa … na kama ana wendawazimu ajaribu kukifuta chama hiki aone moto wa nchi hii,” alisema Mbowe na kuongeza, kuwa labda Tendwa aombe radhi ndipo watamsikiliza.

Mbali na hilo, Mbowe alisema mkakati wa chama hicho wa vuguvugu la mabadiliko utaendelea nchi nzima kwa mujibu wa ratiba.

Alisema Kamati Kuu ilimtangaza Tendwa kuwa adui wa demokrasia na hafai kuwa katika nafasi aliyo nayo ingawa itaendelea kuheshimu Sheria ya Vyama vya Siasa bila kushiriki shughuli zinazosimamiwa na Tendwa.

Mbowe alisema ni lazima viongozi wa Serikali wawe na staha na kutoa kauli zenye busara zisizokuwa na utata, huku akimtolea mfano Msajili kwa kauli alizozitoa hivi karibuni baada ya vurugu za Iringa.

Baada ya vurugu hizo, Tendwa alisema atakifuta chama chochote kinachofanya vurugu zinazosababisha mauaji, kauli ambayo Mbowe alidai kuwa imewafanya wamwone kama anafanya kazi kwa kushinikizwa au kujipendekeza.

“Kumwacha Tendwa aendelee ni kuiingiza nchi kwenye machafuko… Kamati Kuu imeona ni hatari kuendelea naye na imemtaka awajibike kwa kujiuzulu, la sivyo hatutafanya kazi naye wala kupokea amri zake,” alisema Mbowe.

Kuhusu mikutano ya vuguvugu la mabadiliko, alisema chama hicho kimepanga kurudi Iringa ambapo watafanya mikutano katika kila kata na hatimaye mkoani Singida hususani katika jimbo moja ambalo hakulitaja, lakini akasema mikutano hiyo wataifanya kitongoji kwa kitongoji.

Madiwani Mwanza watupwa Wakati huo huo, Chadema imewavua uanachama madiwani wake wawili wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kwa madai ya kukiuka maadili, kanuni na Katiba ya chama hicho kwa kuhusishwa na tuhuma za ufisadi.

Madiwani hao ni Adam Chagulani kutoka kata ya Igoma na Henry Matata wa kata ya Kitangiri ambao walikuwa chini ya uangalizi baada ya Meya wa Jiji hilo, Josephat Manyerere kuvuliwa madaraka na Baraza la Madiwani jijini humo. Kadhalika, chama hicho kimevunja Kamati ya Uongozi jijini humo na sasa kinatarajiwa kuchagua nyingine.

“Baada ya Meya kuvuliwa madaraka hivi karibuni, Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa aliunda kamati ya kuchunguza misingi iliyotumika, iliyojadili na kuridhika na mwisho kuamua kuwawajibisha kwa kuwavua uanachama,” alisema Mbowe na kuongeza kuwa katika hilo, chama hakitaona aibu kwani makosa mengine hayavumiliki.

Alisema wahusika hao waliitwa na walishapewa nafasi ya kujieleza na uamuzi huo wa Kamati Kuu ni onyo kwa viongozi wote wa Chadema.

Alifafanua kuwa chama hicho hakiwezi kumvumilia mtu anayeonekana kukwamisha tumaini la Watanzania kufanikisha ukombozi wa mabadiliko ya kimfumo na kiutawala.

Meya alivuliwa madaraka kwa madai ya kutokuwa na imani naye tangu alipochaguliwa katika wadhifa huo ambapo madiwani 20 walitaka Meya huyo ang’oke na wengine wanane wakasema asiondoke na hivyo kufanya akose sifa.

Mimi si mjomba wa Chadema Akizungumza na gazeti hili kutoka Nairobi jana, Tendwa aliishangaa Chadema kwa kutoa kauli hiyo kana kwamba uhusiano uliopo kati ya chama hicho na yeye ni uhusiano binafsi.

“Mimi sina uhusiano wa ujomba na Chadema, wanakuwa na uhusiano na mimi wa kisheria na nikitoa maelekezo wasipofuata wamevunja sheria … uhusiano wetu si binafsi, kwa uhusiano binafsi hata mimi sina haja nao.

“Hawa wana wanasheria kibao, wameshindwa kuomba ushauri?” Alihoji Tendwa na kutaka vyombo vya habari kutokuwa vya kuchukua wanachosema Chadema, badala yake wawaulize maswali. Akisisitiza msimamo wake, Tendwa alisema kamwe hataiomba Chadema msamaha.

Monday, September 10, 2012

CHADEMA wamshukia JK

• Mkanda wa mauaji wawaliza wajumbe

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemshukia Rais Jakaya Kikwete kikieleza kushangazwa na ukimya wake kuhusu mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa Kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, yaliyofanywa na Jeshi la Polisi.

Akifungua kikao cha Kamati Kuu cha dharura jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema chama hicho kimeshitushwa na kusikitishwa na hali hiyo hasa ikizingatiwa kuwa rais ni Amiri Jeshi Mkuu na kwamba moja ya chombo chake cha dola kimehusika katika tukio la kinyama la mauaji ya mwandishi wa habari.

Alisema inafahamika kuwa Rais Kikwete ni mwepesi kushiriki, kuhudhuria na kutoa salamu za rambirambi katika misiba mbalimbali, lakini katika tukio hili la mauaji ya kusikitisha na kutisha, amekuwa kimya kana kwamba hakuna jambo lolote lililotokea ndani ya nchi anayoiongoza.

“Tunasikitika kama chama katika msiba huu wa mwanahabari ambao umetokea katika mazingira ya kutatanisha na yeye akiwa amri jeshi mkuu, mkuu wa serikali, mkuu wa nchi ambaye majeshi yote yanawajibika kwake, ameweza kuona tukio kubwa kama hili lililogusa hisia za Watanzania mbalimbali, wanadiplomasia, wanaharakati ndani na nje ya nchi na vyombo vya habari vya kimataifa CNN, Al Jazira, lakini Rais Kikwete hajathubutu kutoa kauli.

“Rais yupo Kampala anasuluhusisha mgogoro wa Kongo wakati tuna migogoro ndani ya jamii yetu,” alisema.

Alisema katika siku za hivi karibuni kumeibuka migogoro mbalimbali hapa nchini ikiwamo ya madaktari na walimu na kwamba sasa imeingia kati ya Jeshi la Polisi na wananchi.

Mbowe alisema katika hali hii ya huzuni na hofu kubwa miongoni mwa waandishi wa habari na Watanzania wengi kutokana na kukithiri kwa mauaji ya raia yanayofanywa na polisi, CHADEMA imeshangazwa na kushitushwa na matamshi ya baadhi ya watendaji serikalini ambayo yanajaribu kuficha ukweli wa mauaji na uvunjaji makusudi wa haki za binadamu.

Aliongeza kuwa wakati watu wakiwa katika taharuki kutokana na mauaji hayo, ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya watendaji wa serikali wakiibuka na kutoa kauli zilizojaa uchochezi na kuvunja amani.

Mbowe alitaja moja kwa moja matamshi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, aliyotoa hivi karibuni akitishia kukifuta CHADEMA kwa kile alichosema ni kusababisha mauaji, kuwa ni za hatari na zilizolenga kuonesha kuwa mauaji hayo yanatokana na mgogoro kati ya polisi na chama hicho.

Wamwambia Tendwa ole wako

Mwenyekiti huyo wa taifa na Mbunge wa Hai, alibainisha kuwa wanazo taarifa sahihi zinazoonesha kuwepo kwa mbinu chafu zenye lengo la kukihujumu CHADEMA zinazopangwa na viongozi wa serikali.

Alisema kauli ya Tendwa ya kudai atafuta chama hicho, ni ushahidi tosha wa kuwepo kwa mbinu hizo na kuonya kuwa asijaribu hata sekunde moja kutekeleza mpango huo.

“Kauli za Tendwa zinatishia amani ya nchi na asitishie kukifuta CHADEMA.

“Tendwa acheze na chama chochote kingine, lakini si CHADEMA,” alisema Mbowe.

Walimtaka Tendwa kutambua wajibu wake na kutenda haki ili asiingize nchi katika machafuko.

“Tunataka kutengeneza ushindani wa haki bila kujali tunaingizwa katika matatizo kiasi gani. M4C itaedelea nchi nzima,” alisema.

Wanahabari watiwa moyo

Mbowe aliwataka wanahabari kutokata tamaa kutokana na mauaji hayo, bali tukio hilo liwape ujasiri zaidi katika utendaji wao wa kazi.

“Tukio lile lisiwe mwanzo wa kufifisha juhudi zenu, ila likawaimarishe wanahabari mkijua kwamba mna dhamana kubwa kwa taifa. Na ni sahihi kwamba maisha yetu yapo hatarini hasa pale serikali yetu inapokuwa haichukui hatua za makusudi na za haraka,” alisema.

Pamoja na hilo, aliwapongeza wanahabari waliokuwapo mkoani Iringa wakati wa tukio hilo la mauaji na kuonyesha ushujaa kwa kuendelea kuchukua picha.

“Kwa ujasiri waliouonesha wameiokoa Chadena katika mpango wa kutaka kuchafuliwa…picha hizi ndio zimekuwa salama si kwa CHADEMA tu bali kwa taifa na wanahabari kwa ujumla.

“Tunawashukuru wanahabari pamoja na kumpoteza mwenzao waliendelea kutimiza wajibu wao, wanastahili kupatiwa tuzo nasi kama chama tutawatambua kwa kazi kubwa,” alisema.

Aidha, alisema serikali inasahau kuwa mambo yanayojenga chuki na wananchi kwa serikali yao ni ugumu wa maisha, badala yake wanatumia dola kupambana na wananchi.

Alisema CHADEMA kitaendelea kuwaunganisha Watanzania, kwani bila kuing’oa CCM mwaka 2015 nchi itaingia kwenye machafuko makubwa.

Picha zawaliza wajumbe

Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walishindwa kujizuia na kuangua kilio baada ya kuonyeshwa picha za mnato na video za mauaji ya Mwangosi.

Picha iliyowaliza wajumbe ni ile inayoonekana mabaki ya mwili wa marehemu Mwangosi baada ya kupigwa bomu la machozi tumboni ambalo lilisababisha utumbo kutoka nje.

Kutoa tamko leo

Mbowe alisema baada ya kikao hicho kujalidili suala hilo kwa undani, chama hicho leo kinatarajia kutoa tamko lake.

Alisema katika kikao hicho watajadili kauli za awali za polisi kuhusu tukio hilo, kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Tendwa, Waziri wa Mambo wa Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi na mustakali wa uhuru wa vyombo vya habari.

Pia alisema watajadili utendaji kazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambalo alieleza sasa linatumika kama kipeperushi cha serikali.

“CHADEMA hatutegemei TBC kutengeneza habari, kwani baada ya kuondoka Tido Mhando sasa imekuwa kipeperushi cha serikali. tutajadili mahusiano yetu na TBC na kutoa tamko zito kuhusu hatma yetu na TBC.

“Hakuna ugomvi na waandishi na wapigapicha wa TBC, kwani tunajua wao wanatumwa, bali uongozi. Tukio hili limetokea wao wanapindisha ukweli, wangekuwa na nia nzuri na busara wasingechukua habari za upande mmoja,” alisema.

CUF: Kuuawa mwandishi ni aibu kwa taifa

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa tukio la kuuawa kwa mwandishi Mwangosi ni aibu kwa taifa.

Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, Professa Ibrahimu Lipumba, alisema kuwa mauaji hayo yamelichafua taifa zaidi na ni ishara ya serikali kuwafanya wananchi waogope kueleza mambo yanayowaumiza.

“Kuuawa kwa mwandishi wa habari kwa nchi isiyo na vita ni aibu kwa taifa na kuwafanya wananchi wasiweze kupata habari zinazoendelea katika taifa lao,” alisema.

Kumburuza Nape kortini

Mbowe alisema watamburuza mahakamani Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kutokana na kauli yake kuwa CHADEMA kinapewa mabilioni ya fedha na wafadhili nje ya nchi.

Alisema watampeleka Nape mahakamani ili aende kuithibitisha kauli hiyo na ukweli uweze kubainika.

“Ukifumbia macho hoja hii inaweza kuonekana kuwa ni ya kweli, sasa atakwenda kuithibitisha mahakamani, mahakama ikitenda haki ukweli utajulikana. Wanasheria wetu wanalifanyia kazi suala hili,” alisema.

Kwa muda sasa Nape amekaririwa akisema kuwa chama hicho kimekuwa kikipewa mabilioni ya fedha na wafadhili nje ya nchi na kuwahadaa Watanzania kupitia harambee mbalimbali.

CHADEMA kilimpa siku saba Nape kuthibitisha madai hayo, lakini hakufanya hivyo na kusema kuwa ana ushahidi kuhusu kauli yake dhidi ya chama hicho.

Dk. Slaa afafanua SMS

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa inawezekana IGP, Said Mwema na Waziri wa Mambo ya Ndani, Nchimbi ni mbumbumbu wa sheria kutokana na kudai ujumbe wake mfupi wa maandishi (SMS) ni wa kichochezi.

Alisema kama si mambumbumbu wa sheria, basi hawajui maana ya neno uchochezi na kuhoji kama ujumbe huo ni wa uchochezi kwa nini mpaka sasa hawajamkamata.

“Nilimtumia ujumbe ule IGP, lakini aliupeleka kwa Waziri Nchimbi maana yake anaomba ushauri ambao pia waziri ameshindwa kumpa mpaka mauaji yametokea.

“Nchimbi ameshindwa kutimiza wajibu wake, hivyo anatakiwa kujiuzulu kwa kushindwa kuufanyia kazi ujumbe wa thadhari,” alisema.