Monday, June 25, 2012

Mr Blue apata mtoto wa kiume

Mr Blue apata mtoto wa kiume

HERIETH MAKWETTA
MR Blue ambaye ni miongoni mwa wasanii waliowahi kufanya vizuri kwenye Bongofleva, amepata mtoto wa kiume mwanzoni mwa wiki hii.

Blue amepata mtoto huyo baada ya mchumba wake aliyewahi kumtambulisha kwa jina la Wahida, kujifungua jijini Dar es salaam.

"Nimevuka hatua moja kwenda nyingine. Kwa sasa mimi si mvulana tena ila ni baba, naitwa Baba Sameer," alisema huku akitabasamu.

"Nimeamua kumpa mtoto wangu jina hili maana naona linamfaa, kwani ni jina langu la pili ambalo nimekuwa nikilitumia kwa muda mrefu, pia ni jina la baba yangu."