Askari
wa polisi wa kituo cha kati mjini Nzega,wakikagua viroba vikubwa
vilivyokuwa vimejazwa bangi yenye uzito wa kilogramu 350 na thamani ya
shilingi miloni 5,250,000.Bangi hiyo ilikuwa ikisafirishwa na kijana
Pascal Bangii mkazi wa kijiji cha Bigiri mkoani Tabora kwenda kuuza
Dar-es-salaam.Kijana huyo amehukumiwa kwenda jela miaka 10 baada ya
kukiri kosa.
Kijana
mkazi wa kijiji cha Sigiri wilayani Nzega mkoani Tabora,Pascal Bangii
(31),amehukumiwa na mahakama ya hakimu mkazi mjini Nzega, kwenda jela
miaka 10 baada ya kukiri kosa la kusafirisha madawa ya kulevya aina ya
bhangi yenye uzito wa kilogramu 350 kupeleka jijini Dar-es-salaam kuuza.
Bangi hiyo uliyokuwa imehifadhiwa kwenye viroba vikubwa vinne na nusu,thamani yake ni shilingi 5,250,000.
Awali
mwanasheria wa serikali Maria Mdulungu alidai mbele ya hakimu wa
mahakama ya hakimu mkazi,Chiganga Tengwa kuwa mnano juni 29 mwaka huu
majira ya mchana katika kituo cha polisi cha kati mjini Nzega,mshitakiwa
alikamatwa akiwa na bhangi hiyo akiisafirisha,huku akijua wazi kuwa
kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Mdulungu
alisema siku ya tukio,walipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya
kijana huyo kusafirisha bangi ndani ya basi aina ya youtong T.428 BLR
mali ya kampuni ya Green stars.
Mdulungu
alisema kauli hiyo ya mshitakiwa,iliungwa mkono na kondakta wa basi
hilo na baadhi ya abiria, kuwa mzigo huo haramu wa bangi ni mali ya
mshitakiwa.
Kabla
ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mdulungu aliiomba mahakama hiyo kutoa
adhabu kali ili kuwa fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine
wanaotarajiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya.
Kwa
upande wake mshitakiwa,aliiomba mahakama hiyo imwonee huruma kwa madai
kuwa anayo familia inayomtegemea na kwamba hilo ni kosa lake la kwanza
toka amezaliwa.
Akitoa
hukumu hiyo,hakimu Chiganga,alisema mahakama imezingatia maombi
yaliyotolewa na pande zote mbili,lakini pamoja na maombi hayo,kosa
alilofanya mshitakiwa la kusafirisha baangi ambalo imepigwa
marufuku,halivumikili.
“Madawa
ya kulevya ikiwemo bhangi,ni hatari sana kwa afya za binadamu na hasa
vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.Madawa haya yanapelekea watumiaji
kuwa vichaa.Kutokana na ukweli huo,mahakama hii,inakupa adhabu ya kulipa
faini ya shilingi 15,250,000 na ukishindwa kulipa faini hii,utakwenda
kutumikia jela miaka kumi”,alisema hakimu huyo.
Wakati
mwandishi wa habari hii akiondoka mahakamani hapo,mshitakiwa Pascal
alikuwa hajalipa faini hiyo na hivyo kulazimika kwenda jela kutumikia
kifungo chake.