Kaimu
Mkurugenzi wa manispaa ya Singida,William Haalyakitoa taarifa yake ya
utendaji kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa.
Mkuu
wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi, akifurahia jambo na kaimu
mstahiki meya wa manispaa ya Singida,Pantaleo Sorongai muda mfupi kabla
DC huyo hajaanza kuhutubia wakazi wa manispaa ya Singida (hawapo kwenye
picha)wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku za serikali za
mitaa.Maadhimisho hayo yalifanyika kwenye viwanja vya Ipembe.
Mkuu
wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akihutubia wananchi
waliohudhuria maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa (hawapo kwenye
picha).
Baadhi ya viongozi waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa.
Kikundi
cha burudani cha Nyota njema kikitoa burudani kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa zilizofanyika kwenye viwanja
vya Ipembe mjini Singida.
Serikali
wilayani Singida, imewaagiza madiwani wa manispaa ya Singida
kuhakikisha wanabana mianya yote ya ufujaji wa fedha na mali za umma ili
pamoja na mambo mengine,manispaa iweze kuwa imara kiuchumi.
Wito
huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi,wakati
akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa
zilizofanyika kwenye viwanja vya Ipembe mjini hapa.
Alisema
madiwani wana jukumu kubwa la kuhakikisha lengo la ukusanyaji mapato
linafikiwa na wakati huo huo,fedha zinatumika kama zilivyokusudiwa na si
vinginevyo.
Mlozi alisema hilo liende sambamba na kuwahimiza wananchi kuchangia kwa hali na mali miradi yote ya maendeleo yao.
“Hapa
niwaombe wananchi waondokane na dhana potofu kuwa serikali inao uwezo
wa kuwaletea wananchi wake maendeleo endelevu. Kutokana na na ufinyu wa
bajeti,serikali pekee haiwezi kukidhi mahitaji yote ya kuwaletea
maendeleo wananchi wake.Maendeleo ya kweli,yataletwa na wananchi
wenyewe”,alifafanua DC huyo.
Kauli
mbiu ya maadhimisho hayo ya mwaka huu ni “shiriki sensa ya watu,toa
maoni kuhusu katiba mpya ili kuimarisha ugatuaji wa madaraka kwa
wananchi kwa maendeleo yao”.