Wednesday, July 4, 2012

IJUE SHERIA ;;UNAPOKAMATWA NA POLISI

Mwanaharakati Mzalendo:
Raia ana haki ya
kumwomba askari
ajitambulishe kwako.
Mwulize jina lake
... Mwulize namba
yake ya uaskari
Raia ana haki ya
kujulishwa kwanini
anatiliwa mashaka
ama kukamatwa.
Raia ana haki ya
kuwajulisha ndugu,
jamaa ama sehemu
anakofanyia kazi
kwamba ama
amekamatwa na polisi
ama Taasisi ya Kuzuia
Rushwa.
Raia ana haki ya
kuomba na kupewa
dhamana wakati
akiwa kituo cha polisi
ama Taasisi ya kuzuia
rushwa.
Hutakiwi kutoa
fedha kama
dhamana uwapo
kituo cha polisi
ama Taasisi ya
Kuzuia Rushwa,
isipokuwa maelezo
utakayoandika.
Raia ana haki ya
kuwaeleza polisi ama
Maafisa wa Kuzuia
Rushwa kwamba
lolote atakalosema
linaweza kutumiwa
kama ushahidi
mahakamani, na
asiburuzwe kuandika
tu.
Raia ana haki ya
kuomba Wakili wake
awepo kituo cha polisi
ama Taasisi ya Kuzuia
Rushwa wakati
anatoa maelezo yake.
Raia ana haki ya
kuyasoma kabla ya
kutia sahihi yake.
Raia ana haki ya
kudai risiti ya orodha
ya vitu vyake/fedha
zake alizozitoa ama
kukabidhi kituo cha
polisi ama Taasisi ya
Kuzuia Rushwa.
Raia kama ni
mwanamke ana haki
ya kupekuliwa na
polisi wa kike, na
iwapo hakuna polisi
mwanamke, basi
mwanamke yeyote na
vile vile kwa
mwanamume.
Raia ana haki ya
kufikishwa
mahakamani katika
muda usiozidi saa 24
tangu alipokamatwa
na kufikishwa kituo
cha polisi.