Friday, June 14, 2013

Mzozo mto Nile



Mto Nile

Bunge la Ethiopia, limefutilia mbali mkataba uliosaniwa wakati wa utawala wa kikoloni, ulioipa Misri na Sudan, haki ya kutumia maji mengi ya mto Nile.

Serikali ya Ethiopia, imehoji kuwa mkataba huo ulioidhinishwa mwaka wa 1929, umepitwa na wakati.

Serikali ya Misri, imepinga vikali hatua hiyo na imekasirishwa na uamuzi wa Ethiopia wa kujenga bwawa la maji, katika mto huo wa Nile, ikidai kuwa itapunguza maji yake.

Siku ya Jumatatu rais Mohamed Morsi, alisema hataki vita, lakini anachunguza njia zote.

Awali, nchi sita zilizoko katika eneo la bonde la mto Nile, ikiwa ni pamoja na Ethiopia, zilisaini mkataba ambao unafutilia mbali mamlaka ya Misri ya kuzuia ujenzi wa bwana katika mto Nile.


Chanzo cha Nile
Nile ina vyanzo viwili ndivyo Nile yenyewe (inaitwa pia Nile nyeupe) inayotoka katika Ziwa Viktoria Nyanza na Nile ya Blue inayotoka katika Ziwa Tana . Majina haya ya "nyeupe" na "buluu" yana asili yao katika mji wa Khartoum  ambako mito yote miwili inaunganika ilhali kila moja una rangi tofauti kutokana na udongo tofauti uliotia rangi yake kwenye maji yao.

Chemichemi za Nile ni mito yote inayopeleka maji kwenda Ziwa Viktoria Nyanza katika nchi za Tanzania,Burundi,Rwanda, Kongo, Uganda na Kenya. Chanzo kinachoanza mbali kabisa ni Mto wa Luvironza huko Burundi unaoingia katika Mto wa Kagera  na kufika
Ziwa Viktoria Nyanza

Mkono mwingine wa Nile inaanza Ethiopia ikiitwa Abbai  auNile ya Bluu inatoka katika Ziwa Tana.
Hakuna mapatano kabisa Nile inaanza wapi. Kawaida ya waandisha Waingereza ni kuhesabu kuanzia Ziwa Viktoria; waandishi wa mataifa mengine huwa wanaweza kuita tayari mto wa Kagera kwa jina "Nile ya Kagera".