Wednesday, June 12, 2013

MO PLUS ANAKUJA NA MAKALA WA UKOO VOLUME 1


Ndugu msomaji wa makala hii, leo nimeona ni vyema ni
kufahamishe kuhusu sanaa yetu ya hapa Tanzania amabayo imekua ni moja ya soko la ajira kwa vijana, watoto hata wazee pia.


 
Mo Plus kwa pozi gumu
katika kukuletea makala hii leo nina anza na mwana hiphop na mwanaharakati anaejulikana kama Mo Plus, masikani ni Arusha na shughuli nyingi za muziki anafanyia Arusha.

Wakati napiga nae story, mambo yalikua hivi:-

Manupa: Ulianza lini kujishughulisha na muziki huu wa Hiphop?

Mo Plus: Well,game nimeanza 96 nikiwa o level makumira sec nikiwa na crew iliyoitwa mad gangstaz mpaka 99.

Manupa: Baada ya school pale Makumira nini kiliendelea?


Mo Plus: Baada ya school kila mmoja akawa kimpango coz nilikua na mchz wangu aliyekua anaitwa nasty-b.

Manupa: Ok, vipi ulifanikiwa kwenda A level? kwa maana wanasema wanamuziki hawazingatii masomo

Mo Plus: Nilifanikiwa kuingia A level nikakandamiza alone mpaka chuo IAA,ndipo tukaiunda Kambitata nikiwa na Soja Brain,Papaya tukamuongeza Ntsiki later.

Manupa:Kambitata imeshafanya project ngapi so far?

Mo Plus: Kambitata ilitoa album ya kwanza 2005 iliyoitwa 'IMEANZA' chini ya Banjo Records, producer akiwa Warback pia after college kutokana na distance harakati zikafifia dzain japo crew ipo.

Manupa: ukiwa kama mwanahiphop unaejitegemea umeshafanya kazi za peke yako?

Mo Plus: Well, 2011 feb nilitoa mixtape yangu ya kwanza iliyoitwa 'BABA WA UKOO VOLUME 1', iliyokua na ngoma kama Hizi flow,Hiphop Movement, chini ya Dx wa Noizmekah studio ambaye ndio main producer wangu hadi sasa pia nimefanya kazi na studio kibao na maproducer tofauti kama John B ,samtimba,Q,Kz,Daz Knowledge na wengineo ,

Manupa: Vipi kwa sasa una project yeyote unafanya kuhusu hiphop?

Mo Plus: Ok, sasa hivi nadili na mixtape ya MAKALLA WA UKOO VOL 1, nikiwa na mwanangu JCB,mixtape hii itakua mtaani very soon so watu wangu wa stay tuned for it.

Manupa: asante kwa time yako Mo
Mo Plus: Pamoja sana Manupa.

 

Huyo ndio Mo Plus a.k.a baba Malcom, bonyeza hii link usikilize moja ya kazi zake alizofanya





Pia unaweza kuangalia baadhi ya video alizofanya huyu hiphop master toka arachuga


pia kuna nyingine hii hapa ina Sixteen