TUJIFUNZE
UCHUMI/BIASHARA
ELEWA MAMBO YA FEDHA ILI UJENGE UTAJIRI
· PESA
· AKIBA
· VITEGA
UCHUMI
· MIKOPO
· UWEKEZAJI
KATIKA HISA
· UWEKEZAJI
KATIKA HATI FUNGANI
· MCHANGANUO
WA MAZINGIRA (BUSINESS ENVIRONMENTS)
· KUPANGA
MIPANGO YA FEDHA
· UWEKAJI
HESABU ZA FEDHA
· KUDHIBITI
HATARI/MASHAKA KATIKA BIASHARA
· WATOA
HUDUMA ZA FEDHA
· MPANGO
KAZI
1.
PESA
· Pesa
inapotajwa, kitu gani kinakuja kwenye fikra zako?
· Pesa
ni nini?
Pesa
ni chombo cha mabadilishano.,ni thamani inayolingana na bidhaa au huduma
iliyobadilishwa na ni fedha halali inayokubalika kwa wananchi wan chi
husika.Pesa inatumika kununulia bidhaa na kulipia matibabu,Ankara za simu na
umeme au mishahara ya wafanyakazi.Pesa pia inatumika kama kiwango cha thamani
cha kupimia thamani ya bidhaa na huduma mbali mbali.Idadi ya vipande vya pesa
vinavyotakiwa kununua bidhaa ndio bei ya bidhaa yenyewe.
Pesa
pia hutumika kama hifadhi ya thamani ya uzalishaji wa leo wa bidhaa na huduma
kwa matumizi ya baadaye.Inawezekana kuwa usumbufu kuweka stoo uzalishaji wa
ziada na mara nyingi watu huuza na kuweka pesa wanazopata benki au taasisi
nyingine za fedha.Pia wanaweka akiba kwa kununua mali (kama ng’ombe,nyumba,hisa
n.k.)
1.1
Chimbuko
la pesa
· Watu
walikuwa wakibadilishana vipi bidhaa hapo kale?
· Pesa
imetokea wapi?
Historia ya pesa ni ya miaka maelfu nyuma.watu
walizoea kubadilishana bidhaa kupitia biashara ya kubadilishana vitu. Katika
uchumi wa kubadilishana mali, mtu mwenye kitu cha kuuza lazima kwanza atafute
mtu mwenye kitu kinachokubalika kutolewa ili kibadilishwe.Kwa mfano, mtu
angeweza kubadilishana mbuzi wawili kwa gunia moja la mahindi
Muda ulivyosogea, watu wakaanza kutumia vito,
chumvi, viungo, pembe za ndovu na makombe kuwakilisha thamani ya vitu
vinavyouzwa.Matumizi ya kauri au pembe za ndovu yalikuwa karibu kila mahali
kabla binadamu hajagundua jinsi ya kufua madini ya thamani kama vile dhahabu na
fedha kuwakilisha thamani ya bidhaa zinazouzwa.Madini haya baadaye
yalitengenezwa sarafu na thamani ya sarafu iliamuliwa kwa ukubwa wake.
Katika uchumi wa pesa, mwenye bidhaa anaweza kuiuza
kwa pesa, ambayo inakubalika kwa malipo ya bidhaa, kwa hiyo kuepuka muda na
juhudi ambazo zingehitajika kumtafuta mtu ambaye atafanya biashara
inayokubalika. Pesa ya kisasa iko kwenye mfumo wa sarafu au noti za benki.Pesa
ya karatasi ndio mfumo unaotumika zaidi wa pesa halisi.Mfumo mwingine wa pesa
ni pesa ya mkopo, ambayo mara nyingi iko kwenye mfumo wa kadi za plastiki (kama
vile card za pesa,kadi za mashine za kutolea pesa (ATM)). Pesa ya mkopo
inadhaminiwa na ahadi ya mtoaji (iwe ni serikali au taasisi yoyote ya kifedha)
kulipa thamani inayolingana katika kiwango cha pesa ya chuma, kama vile dhahabu
au fedha.Pesa ya karatasi haibadilishiki kwenye aina nyingine yoyote ya pesa na
thamani yake hupangwa na mamlaka ya serikali.
1.2
Sifa
bainifu za pesa za kisasa
· Ni
ndogo na inabebeka kiurahisi
· Inaweza
kugawanywa kwenye sehemu ndogo ndogo
· Inadumu
· Inakubalika
na wote
· Inarahisisha
biashara
1.3
Kwa
nini tunahitaji pesa?
Hatuwezi
kuzalisha kila kitu tunachohitaji au kufanya kila kitu.Tunahitaji watu wengine
wazalishe baadhi ya vitu na kutupatia baadhi ya huduma.Kwa hiyo, tunahitaji
pesa ya kununulia bidhaa hizo na kulipia huduma hizo.
Tunahitaji
pesa kwa kubadilishana na kile tunachohitaji.tunahitaji pesa inayoendana na
mfumo wa maisha yetu
1.4
Tunaipataje
pesa?
Tunaweza kupata pesa kupitia njia zifuatazo:
·
Kufanya
kazi kwa mshahara au ujira
·
Kuwapatia
watu wengine huduma zetu
·
Kilimo
na kuuza bidhaa mbali mbali
·
Kufanya
biashara
·
Michango
au ruzuku kutoka kwa ndugu,marafiki na wengine
·
Pensheni,bonasi
na aina nyingine ya fidia
·
Gawio
kutokana na akiba kwenye chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) au hisa kwenye
kampuni zilizomo kwenye soko la hisa la Dar es salaam
1.5
Tunatumiaje
pesa
Tunatumia
pesa kwa:
· Matumizi
ya kawaida
· Kuweka
akiba
· Kitega
uchumi
1.6
Ni kwa namna gani matumizi ya fedha huleta tofauti?
Pesa kama chombo cha kubadilishana,kinaweza
kutumika kuongeza uzalishaji au matumizi.pesa inayotumika kununulia matumizi ya
kawaida haiongezi mapato ya baadaye.pesa iliyowekezwa au akiba kwa kitega
uchumi cha baadaye inaweza kuleta mapato zaidi.
2. Akiba
2.1
Akiba ni nini?
Akiba ni pesa au mali za thamani zinazowekwa
pembeni au kutunzwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye.zinaweza kuwa kwenye mfumo
wa pesa taslim, mifugo,chakula n.k. Akiba hutumika nyakati za upungufu au
dharura ikitokea.
Kuweka akiba ni kitendo cha makusudi cha kuacha
kutumia pesa kwa sasa na kuiweka pembeni kwa matumizi ya baadaye
2.2
Tunawekaje akiba?
Tunaweza kuweka akiba kwa kuweka pesa kwenye akaunti ya
benki ya biashara,akiba na hisa kwenye chama
cha kuweka
na kukopa (SACCOS) au benki imani au VICOBA au michango ya kupokezana kwa jina
lingine
mchezo
(ingawa kisheria sio rasmi).watu wengine wanaweka pesa zao kwenye mifuko ya
plastiki (tena ndo
wengi kwa
sasa hasa wafanyabiashara wa kihindi) na kuificha chini ya kitanda,kwenye
mto,nyufa za nyumba
au kwenye
mti.tunaweza pia kuhifadhi mazao kwa matumizi ya baadaye wakati mahitaji
yanapokuwa ni
makubwa.
2.3
kwa nini tunahitaji kuweka akiba?
Vyanzo vya mapato havitabiriki au ni vya msimu hasa
kwa watu wanaotegemea ajira au kilimo au hata wafanyabiashara.inatubidi
tutarajie matatizo na dharura kiasi fulani kwenye maisha yetu.Akiba inatukinga
kutokana na kutumia tukiwa tuna kipato kidogo au hatuna kabisa.tunaweka akiba kwa
ajili ya mahitaji ya mzunguko wa maisha kama vile kuzaliwa kwa mtoto na kukidhi
mahitaji ya mahali pa kuishi na dharura nyingine kama ugonjwa au kwa mahitaji
ya kuwekeza.
2.4
changamoto za aina mbali mbali za akiba
Ni
nini faida na madhara ya kuweka pesa nyumbani, benki,SACCOS,mzunguko au kitega
uchumi?
2.4.1 kuweka
nyumbani
ni hatari sana kuweka nyumbani pesa kwani inaweza
kuibwa haraka na kwa urahisi sana.inaweza pia kuliwa na panya,wadudu kama mende
au hata kuungua.pia inaweza kutumika kwa matumizi yasiyo ya lazima.katika
mifumo ya kifamilia inaweza kutumika vibaya na wanandoa walevi,watoto au hata
ndugu wengine wa familia
2.4.2 akaunti
za akiba kwenye benki
mabenki yana masharti magumu hasa kwa wale
wanaotaka kukopa pesa.aidha, masharti na vigezo vinaweza kuwazuia watu wengi.pia,gharama
za huduma za kibenki ni za juu sana
2.4.3 SACCOS
Ili kuendesha SACCOS mtu anahitaji kuwa na
mtiririko thabiti wa mapato kwani michango hufanyika mara kwa mara.uzalishaji
kipato miongoni mwa watu hautabiriki na unaweza kukwamisha juhudi za kuweka
akiba
2.4.4 Mzunguko
(mchezo)
Katika utaratibu wa mzunguko,mwanachama mmoja wa
zamu yake na baadaye akakataa kutoa michango kwa wengine.kikundi pia kinaweza
kuvunjika kabla ya mzunguko kukamilika.
3. vitega
uchumi
watu wana mahitaji mengi zaidi kuliko ambavyo
rasilimali zao finyu zinavyoweza kukidhi.wanataka kununua au kujenga
nyumba,kununua kipande cha ardhi,kununua chakula,kulipa karo za shule au kuweka
pesa kidogo kwa matumizi ya baadaye.pesa huwa haitoshi kufanikisha matakwa yote
haya.kutumia pesa kwenye kipengele kimoja ina maana hakuna itakayopatikana kwa
ajili ya kingine
tofauti katika utajiri wa watu ,hata kama
wanaingiza kipato sawa,kunategemea maamuzi yao ya kutumia pesa.wengine
wanapendelea kutumia pesa kwa ajili ya vitu vya anasa vya kila siku kuliko
kujipatia mali ili kuzalisha kipato zaidi hapo baadaye.uchaguzi wa kutumia pesa
ambao hufanywa na mtu sasa hivi ndio utakaoamua hali ya kifedha hapo
baadaye.mtu anayeweka pesa kwenye shughuli inayozalisha atakuwa na kipato zaidi
hapo baadaye.
3.1
uwekezaji ni
nini?
Uwekezaji ni kuacha matumizi ya leo kwa ajili ya
shughuli ambayo itakuingizia kipato zaidi hapo baadaye.hii ina maana kwamba
unachagua kutokutumia pesa yako kwenye chakula,nguo,starehe badala yake
unanunua mali ambayo itakuingizia kipato zaidi.uwekezaji maana yake ni kutumia
pesa yako katika njia ambazo zitaongeza uwezo wako wa kuingiza kipato.hii
inajumuisha kuanzisha au kupanua biashara,kununua mifugo,kununua shamba,kujenga
nyumba kwa ajili ya kupangisha,kuwaelimisha watoto n.k.
3.2
tofauti kati ya uwekezaji na akiba
akiba unaweka pesa pembeni kwa matumizi ya
baadaye.unaweza kuweka kidogo kidogo hadi kufikia kiasi cha limbikizo kuu
uwekezaji ni kuweka pesa kwa ajili ya shughuli za
uzalishaji.madhumuni ni kuzidisha ulichokuwa nacho leo kwa siku zijazo
3.3
aina za vitega uchumi
3.3.1
vitega uchumi vya muda mfupi
pesa inayowekezwa inatarajiwa kurudisha matokeo
(kipato) karibuni.muda unaochukua kabla ya matokeo yanayotarajiwa kupokelewa
kawaida ni chini ya miaka miwili.vitega uchumi vinajumuisha kuanzisha biashara
n.k
3.3.2 vitega
uchumi vya muda wa kati
hivi ni vitega uchumi vinavyochukua miaka kadhaa
kabla ya kuanza kupata kipato kutokana navyo.pesa inatarajiwa kuanza kutiririka
baada ya miaka miwili;inaweza yote kuja kwa mkupuo au mtiririko wa pesa wa mara
kwa mara.mifano, inajumuisha ununuzi wa hisa za kampeni kwenye soko la hisa
(stock exchange market) ili kupata gawio au kuendeleza shamba lako kuongeza
uzalishaji
3.3.3 vitega
uchumi vya muda mrefu
hivi ni vitega uchumi ambavyo vinahitaji pesa
nyingi zaidi na kuchukua muda mrefu kukamilisha mradi.mapato yake yanaweza
kuanza kutiririka baada ya kukamilika kwa mradi lakini itachukua muda mrefu
kabla ya kupata pesa uliyowekeza kwenye mradi.muda utakaochukua kupata pesa
yako ni mrefu.vitega uchumi hivi hujumuisha uwekezaji kwenye majengo,kuwapatia
watoto elimu,ununuzi wa shamba n.k.
faida ya vitega uchumi vya muda mrefu ni kwamba
baada ya muda huongezeka thamani.hii ina maana kwamba ukiwa na kitega uchumi
sahihi,utajiri wako utaongezeka wakati ujao.
3.4
kwa nini tuwekeze?
Tunawekeza ili:
·
kujenga
utajiri
·
kuongeza
uwezo wa kupata kipato zaidi
·
kuanzisha
fursa za kuzalisha kipato uzeeni
·
kutengeneza
ajira kwetu wenyewe na familia
3.5
wapi na
jinsi gani tunaweza kuwekeza?
Kwa kawaida watu wanawaiga wengine wakati
wakiwekeza pesa zao.ninafungua biashara ya nguo kutoka uchina,na wewe pia
unaamua kufungua biashara ya nguo kutoka uchinia.haya ni makosa.unahitji ufanye
tathmini ya fursa mbadala zilizopo.fikiria kitahitajika kitu gani kutoka kwako
na kama unaweza kumudu.
3.5.1
jinsi ya kufanya maamuzi ya kuwekeza
kuna njia nyingi unazoweza kuchagua za kuwekeza
ambazo,hata hivyo,hazitaweza kukupa matokeo kama ambavyo ungependa.vifuatavyo
ni baadhi ya vitega uchumi ambavyo unaweza kuwekeza pesa yako kutegemea na
mahali ulipo:
·
kuwekeza
kwenye mali ambazo zinapanda thamani kama vile ardhi
·
kuwekeza
kwenye miradi/mitaji ya biashara ukitarajia itaongezeka thamani hapo baadaye –
hisa.
·
Kuwekeza
kwenye mali ambazo zinaanza kuingiza mapato mara moja, kama vile kuanzisha duka
au hoteli
·
Kuwekeza
kwenye mali ambazo hutoa huduma kwa watu wengine kama vile gari dogo au basi la
kubebea abiria au mizigo
·
Kuwekeza
pesa kwenye biashara za ubia,kama vile kuanzisha kampuni au ushirika.unapaswa
kufanya kazi na watu unaowaamini
·
Kuwekeza
kwenye zaidi ya mradi mmoja, kama vile kuwa na shamba na duka kutapunguza
hatari ya kufilisika.
Ni muhimu kuzingatia kuwa pesa hupoteza thamani
jinsi muda unavyokwenda hasa pesa yetu ya kitanzania.iwapo una shilingi leo
unaweza kununua vitu vingi zaidi kuliko utakavyoweza baada ya mwaka mmoja.pesa
inadumisha thamani yake ya uwiano inapowekezwa kwenye shughuli ya kuingiza
kipato.pesa yako inapaswa ikuingizie kipato wakati wote.
Ili uweze kufanya tathmini ya uwekezaji wako
inabidi ukokotoe uwiano wa pesa yako itakavyokuwa hapo kesho na mapato unayotaka
kuingiza.kama pesa yako itapoteza kwa 10% kila mwaka hii ina maana kwamba
shilingi 100 yako leo,itakuwa sawa na shilingi 110 mwaka kesho wakati huu.kwa
hiyo kama unataka kuwekeza shilingi 100 kwa mwaka mmoja inapaswa iwe zaidi ya
110 kwa mwaka ujao,angalau kwa thamani yake kubaki vile vile.kiasi chochote
chini ya hapo ni hasara kwako.