Friday, June 21, 2013

CUF yaomba kuongoza kambi rasmi ya upinzani bungeni.


Akiomba mwongozo wa Spika bungeni mapema leo,Mbunge wa Lindi Mjini Mhe Salum Halfan Barwani(CUF) amemtaka Spika wa Bunge Anne Makinda kutoa mwongozo na kuruhusu chama cha Wananchi CUF kuongoza kambi rasmi ya upinzani Bungeni kutokana na Wabunge wa CHADEMA kutokuwepo bungeni.

Baada ya kipindi cha maswali na majibu kuisha leo asubuhi, Mbunge wa Lindi mjini kupitia Cuf mh Baruani,amesimama na kuomba muongozo kwa mh.Spika akiomba sasa kwa vile kambi ya upinzani haipo bungeni na eneo lao kuwa wazi anamtaka spika kuruhusu mapinduzi kwa chama chake cha Cuf kuongoza kambi hiyo kwa sasa.

Mh Makinda akijibu muongozo huo kwa umakini tofauti na alivyo zoeleka kuegemea matakwa na sio kanuni amejalibu kueleza utaratibu wa kuunda kambi ya upinzani bungeni ambapo amesema kuwa mwaka 1995 chama cha NCCR Mageuzi waliunda kambi ya upinzani baada ya kutimiza asilimia 30 ya wabunge wao wakati, huo pia ameeleza mwaka 2000 Cuf waliunda kambi yao wenyewe pia,lakini mwaka 2005 kambi rasmi ya upinzani iliundwa na vyama vyote vya upinzani baada ya kuonekana kuwa Cuf wakati huu hawakutimai asilimia zilizokuwa zinahitajika ikabidi busara ya Spika wa wakati huu 'Very interesting ' hapa akabadili utaratibu badala ya asilimia 30,ikabadilishwa na kufika asilimia 12 hivyo kufanya upinzani kukidhi vigezo na kuunda kambi yao wote bili kujali vyama vyao amesema pia Spika wa wakati huu alitumia Diplomasia kuwaomba Cuf kuunda kambi na vyama vingine.

Kwa mwaka 2010 yeye alichofanya ni kutafasili nini maana ya kambi ya upinzani ambapo kwa mujibu wa Makinda anasema kambi ya upinzani ni vyama vyote vya upinzani vyenye wabunge ndani ya bunge,na kushangaa ni kwa nini Chadema hakijawajumuisha wenzao ndani ya kambi hii,akasema kwa sasa Cuf kikanuni hawawezi kuchukua kambi hiyo make Cdm hawajiarufu kiti kama hawaendelea kuwa kambi rasmi ya upinzani,hayo ndio yaliyojiri asabuhi hii Mjengoni.