Wednesday, May 29, 2013

Watu kukusanyika Leaders kujipanga kumpokea marehemu NGWAIR



Afande Sele
Wadau na wasanii wote mlioguswa na msiba, Kesho saa kumi kamili tukutane leaders club kujipanga kupokea na Kuendesha msiba wa ALBERT MANGWAIR kwa kamati ya Wasanii, M to the P nae hatunae! Ngumu kuamini ila kifo ni kwa kila kiumbe hai wapumzike kwa amani.

Lady Jaydee
KUHUSU TAMKO LA MSANII LADY JAYDEE LA SHOO YAKE YA MIAKA 13,ILIYOKUWA IFANYIKE IJUMAA HII.AMESEMA KUPITIA KIPINDI CHA SUPAMIX YA EAST AFRICA RADIO KWA UCHUNGU MKUBWA KUWA SHOO HIYO HAITOFANYIKA TENA KUTOKA NA KIFO CHA MSANII NGWAIR MPAKA PALE TAREHE NYINGINE ITAKAPOTAJWA TENA#RIP NGWAIR


P Funk Majani

Producer mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya P Funk Majani amefunguka na kusema hataki kusikia Stesheni ya Clouds fm ikipiga wimbo wowote Marehemu Mangwear uliotengenezwa kwenye studio yake ya Bongo Records ukichezwa kwenye kituo hicho.

Kwenye SmS aliyoituma na binafsi kuipata Producer huyo ameanza kwa kutoa rambirambi zake na kumuelezea Ngwear kwake yeye kama moja kati ya nyota ing'aayo

Akiendelea na kuonyesha kuushtumu Uongozi wa kituo hicho kwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine kwa kumsababishia msongo wa kimawazo uliompelekea kuanza kutumia madawa ya kulevya kitu ambacho inaaminika ndicho kilichosababisha kifo chake.
Joh Makini
Kutokana na msiba huu mzito nimesogeza mbele kuachia ngoma yangu mpya pamoja na show yangu club 71 tegeta mpaka nitakapowatangazia tena,Huzuni.


Ujumbe wa P funk