MITAZAMO YA MANUPA

Pages

  • Home
  • Music Stories
  • Jifunze Kinyiramba
  • Afya na Mahusiano
  • Michezo/Sports-
  • Jifunze Kinyisanzu
  • Jokes Corner

Thursday, May 23, 2013

Rais Kikwete atoa tamko kali, vurugu Mtwara


 Rais Jakaya Kikwete amekemea vikali vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara kusini mashariki mwa Tanzania baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Akizungumza mjini Dodoma, Rais Kikwete amesema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali. Aliongeza kuwa rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote. Akizungumza bungeni jana Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema mradi wa kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, umeanza kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda huko wiki ijayo kuweka jiwe la msingi. Tamko hili la Muhongo ndilo lililoibua vurugu kubwa Mtwara. Aidha jambo lingine linalosemekana limesababisha ghasia hizo ni hatua ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutokurusha moja kwa moja matangazo ya Bunge hivyo kuwakosesha wananchi fursa ya kusikiliza bajeti hiyo. Baadhi ya duru zinasema mtu mmoja amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kutokana na vurugu hizo. Milio ya risasi za moto na mabomu ya machozi vilisikika katika maeneo kadhaa ya Mtwara ambako hali ilikuwa mbaya kutokana na kuzuka mapambano kati ya polisi na vijana waliokuwa na hasira.
Posted by Unknown at 11:29:00 AM
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Newer Post Older Post Home
Powered By Blogger

My links

  • Singida connection facebook group
  • Singida connection
  • soundcloud

Vistors

Followers

About Me

Unknown
View my complete profile

BLOG ARCHIVES

  • June (1)
  • May (1)
  • September (20)
  • August (18)
  • July (2)
  • June (60)
  • May (42)
  • December (2)
  • October (6)
  • September (46)
  • August (116)
  • July (282)
  • June (92)

Blog zingine

Popular Posts

  • MASWALI NA MAJIBU JUU YA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA
       Je ni kweli kuwa madhara ya uvutaji moshi wa sigara yako ni kidogo kuliko yale yatokanayo na kuvuta? Kama nitasimama karibu na mvutaji ...
  • SIKILIZA NYIMBO YA KINYIRAMBA YA IRIEMNAS SANGA
    Iriemnas Sanga ni mtanzania nayeishi Finland, huko anajishughulisha na mambo mbalimbali ikiwemo sanaa ya music, hiki ni kibao chake, unawez...
  • Ufisadi fedha za JK watikisa Bunge
    UFISADI wa fedha za Serikali zaidi ya sh bilioni tatu zilizotengwa kwa ajili ya safari za nje za Rais Jakaya Kikwete, zimelitikisa Bunge. M...

Online

DFM. Powered by Blogger.