JESHI la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia Tausi Kapera (24) mkazi wa Njia Nne, Ngerengere, kwa tuhuma za kuwanywesha watoto wake sumu ya panya, pamoja na yeye mwenyewe kwa lengo la kutaka kujiua, baada ya kutokea ugomvi kati yake na mume wake.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, aliwataja watoto hao kuwa ni Abdulazizi Hamisi (mwenye umri wa mwaka mmoja na miwezi mitatu) na Ramadhani Khamisi (6).
Alisema Tausi alitenda kosa hilo juzi, saa 12 jioni, huko Njia Nne, Ngerengere.
Alisema kabla ya kunywa sumu hiyo, alianza kuwanywesha watoto wake, kisha naye akanywa, chanzo kikiwa ni ugomvi kati yake na mume wake, Khamisi Asan, ambaye ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 121 KJ Sangasanga.
Alisema watoto hao pamoja na mama yao, wamelazwa katika Kituo cha Afya Ngerengere, kwa ajili ya matibabu, huku mwanamke huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Alisema atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo, baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali.
Wakati huo huo, mtoto Dotto Shabani (6) mkazi wa Fulwe Wilaya ya Morogoro, amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari wakati akijaribu kuvuka barabara.
Alisema tukio hilo, lilitokea juzi saa 6:30 mchana, katika eneo la Fulwe, barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam.
Alisema mtoto huyo, aligongwa na gari lenye namba za usajili T 964 BWU, mali ya Kiwanda cha Sukari Mtibwa.
Alisema gari hilo, lilikuwa likiendeshwa na Salum Komo (28), mkazi wa Mtibwa Turiani, likitokea kijiji Cha Msolwa kuelekea Turiani.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva huyo kutojali watumiaji wengine wa barabara na kwamba amekamatwa, anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi kukamilika.