Mkuu
wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone, akitoa amri halali ya kupiga
marufuku wanunuzi binafsi kununua Alizeti kwa wakulima na badala yake
kazi hiyo itafanywa na vyama vya msingi vya ushirika.
Baadhi
ya waandishi wa habari (walioketi mbele) na viongozi wa vyama vya
msingi vya ushirika mkoani Singida wakimsikiliza mkuu wa mkoa Dk.Parseko
Vicent Kone (hayupo pichani) akitoa amri halali ya kupiga marufuku
wanunnuzi binafsi kununua alizeti.Kazi hiyo ya ununuzi wa zao la
Alizeti,sasa itafanywa na vyama vya msingi vya ushirika pekee.Lengo ni
mkulima kunufaika na kilimo cha zao hilo.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone, amepiga marufuku wanunuzi binafsi kununua zao la alizeti kutoka kwa wakulima.
Amri hiyo halali,imeanza kutekelezwa kuanzia juzi msimu huu wa mwaka 2011/2012 na kuendelea.
Dk.Kone ametoa amri hiyo halali,juzi wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi yake mjini hapa.
Alisema
lengo la amri hiyo, ni kutoa fursa kwa vyama vya ushirika kuwa wanunuzi
pekee wa zao hilo la alizeti ambapo msimu uliopita,liliingizia mkoa
pato la zaidi ya shilingi bilioni sita.
Dk.Kone
alisema serikali mkoani Singida,imefikia uamuzi huo baada ya kubaini
kuwa wanunuzi binafsi wamekuwa wakiwanyonya wakulima kwa kununua alizeti
kwa bei ndogo sana.
“Pia
mkoa umekuwa ukikosa takwimu sahihi za uzalishaji wa alizeti na mbaya
zaidi, wanunuzi wamekuwa wakitorosha zao hili kwa njia ya panya, hivyo
mkoa kukosa pato litokananlo na alizeti”,alisema Dk.Kone.
Alisema
mfumo wa stakabadhi ghalani unaotumiwa na vyama vya msingi vya
ushirika, ndio mfumo pekee ambao unaweza kumsaidia mkulima mdogo kupata
pato linalolingana na jasho lake.
”Lengo
kuu la muda mrefu la maendeleo ya Tanzania kwa kizazi kijacho kama
ilivyoainishwa kwenye dira ya maendeleo ya Tanzania 2025, ni kupatikana
kwa maendeleo endelevu ya binadamu.Kwa hiyo, ushirika ni mojawapo ya
nyenzo kukufanikisha dira hiyo”,alisema.
Mkuu
huyo wa mkoa, alitoa amri hiyo,alisema “kuanzia juni 21 mwaka huu, na
kuendelea vyama vya ushirika vya msingi, ndivyo pekee vitaruhusiwa
kununua zoa la alizeti toka kwa wakulima.Wanunuzi binafsi, watanunua
alizeti kwenye maghala kwa maelekezo ya chama kikuu cha ushirika, SIFACU
na kwa bei watakayokubaliana”.
Mkutano
huo wa mkuu wa mkoa wa waandishi wa habari, ulihudhuriwa pia na
mwenyekiti wa SIFACU Omari Nyuda na viongozi wa vyama vya ushirika 551.