MBUNGE wa Viti Maalum, Al-shaymaa Kweigyir (CCM), jana aliangua kilio
bungeni kutokana na kukithiri vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu
wa ngozi (albino), huku akiitupia lawama Serikali kwa kushindwa kuchukua
hatua kali dhidi ya watu wanaohusika na mauaji hayo.
Kweigyir aliangua kilio hicho, alipokuwa akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ya mwaka 2012/13, ambapo alisema Serikali imeshindwa kukabiliana na mauaji hayo.
“Inasikitisha jamani, Serikali imeshindwa kuchukua hatua dhidi ya watu ambao wanawaua albino bila hatia….wamekuwa wakiwaua albino wasiokuwa na hatia mpaka sasa idadi ya vifo imeongezeka na kufikia 80 nchini kote.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, wewe ndiyo mtu wa kutusaidia sisi walemavu wa ngozi, lakini umekaa kimya, hivi karibuni aliuawa faru ajulikanaye kwa jina la George na watu waliohusika na mauji hayo walikamatwa, kwa nini wauaji wa maalbino hawakamatwi.
“Hivi karibuni ameuawa albino huko wilayani Arumeru, hata alipogundulika kuwa ameuawa tayari alikutwa amekatwa viungo mbalimbali mwilini, ikiwemo sehemu za siri, kwa hali hii siungi mkono hotuba hii ya Waziri Mkuu, hadi nipate majibu,” alisema huku akihoji Mbunge huyo.
Mbunge huyo, ambaye pia ni mlemavu wa ngozi, alisema ni muhimu Serikali ikaweka alama maalum barabarani ambazo zitawaelekeza madereva kuweza kuwatambua watu wenye ulemavu wa viungo, wakiwemo wasiosikia na wa macho ili wavuke kwa urahisi.
Hata hivyo, mbunge huyo alishindwa kujizuia na kujikuta muda wote, akibubujikwa na machozi, hali iliyomfanya ashindwe kuendelea, huku Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, akimbembeleza na kumtoa nje ya ukumbi wa Bunge.