WAKATI mgomo wa madaktari ukiendelea nchini, Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza ahadi yake aliyoitoa
mwishoni mwa Februari mwaka huu kwamba mgomo wa madaktari hautatokea
tena nchini.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mkurugenzi Mtendaji wake, Dk. Hellen Kijo-Bisimba, kituo hicho kimeilaumu Serikali kwa ujumla kwa kutokuwa makini katika kushughulikia masuala ya madaktari walioko kwenye mgomo.
Kimesema kwamba Serikali imeshindwa kutoa taarifa kwa umma kuhusu tume iliyoundwa kati ya madaktari na Serikali kuhusu utatuzi wa mgogoro huo.
Kimetaka Serikali ihakikishe kwamba vifaa vya tiba na madawa muhimu katika vituo vyote vya afya vinapatikana ili wananchi wote waweze kupata huduma bora za afya.
“Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa inatekeleza kwa dhati Makubaliano ya Abuja kwa kuhakikisha kweli inatenga asilimia 15 ya bajeti yake katika kuboresha huduma za afya. Hiyo itasaidia katika kuondoa matatizo yanayoikabili sekta hiyo hivi sasa,” kimesema.
Kimeongeza: “Serikali imekuwa ikiendelea kuongelea kuboresha maslahi ya madaktari bila kuzungumzia suala la uboreshaji wa huduma za afya na upatikanaji wa vifaa vya tiba.”
Kituo hicho kimeitaka Serikali ichukue hatua za dhati katika kuzuia mgomo mwingine wa madaktari kwa kuwa wanaoathirika ni wanachi wasio na kipato, wasiowweza kutibiwa kwenye hospitali binafsi na wasioweza kutibiwa nje ya nchi.
“Mamlaka zote za nchini zitambue, ziheshimu na kuwajibika kwa wananchi walioziweka madarakani kwa mujibu wa ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” kituo hicho kimesema.
Kimetaka umma wa Watanzania kuamka kudai na kuikumbusha Serikali kuwa inawajibika kwa watanzania na si kwa kikundi kidogo cha watu wanaolinda maslahi yao.