Monday, June 3, 2013

Kuhusu mauzo ya ringtones za Ngwair

 
 Tamko la Push Mobile na Bongo Records kuhusu mauzo ya ringtones za Ngwair
Kufuatia maswali mengi ambayo yamejitokeza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu uuzwaji wa nyimbo za marehemu Albert “Ngwair” Mangwea kupitia mitandao ya simu ambayo ni wadau wetu wakuu katika biashara hii, tumeona ni vyema tuweke bayana kwa wadau na wapenzi wa Mangwea kuwa:

“Kampuni ya Push Mobile na Bongo Records ndio wasambazaji halali wa kazi za Mangwea katika mitandao ya simu. kwa makusudio mema kabisa tunawaomba mashabiki wake mnunue nyimbo zake kwa wingi, zinazopatikana kwenye mitandao ya simu kupitia “CODE MAALUMU” ikiwa ni njia mojawapo ya kumuenzi na kuhakikisha kuwa muziki wake unaishi daima ili familia yake iweze kufaidika na kazi zake.

Sisi kama wadau wakubwa wa pamoja tumetoa TZ milioni 10 na kwa sababu nimbo za marehemu ziko kwenye mitandao kwa muda mrefu, basi tumeona huu ni wakati muafaka kuwajulisha mashakiki wake kumuenzi kwa kuzinunua ambapo mapato ya nyimbo hizo kupitia mitandao ya simu yatapelekwa moja kwa moja kusaidia familia yake.”

Pia tunawahimiza kutoa michango yenu kupitia kamati maalum ya maandalizi ya mazishi ambayo sisi pia ni wajumbe) au kwa kununua nyimbo zake