MITAZAMO YA MANUPA

Pages

  • Home
  • Music Stories
  • Jifunze Kinyiramba
  • Afya na Mahusiano
  • Michezo/Sports-
  • Jifunze Kinyisanzu
  • Jokes Corner

Thursday, May 23, 2013

Rais Kikwete atoa tamko kali, vurugu Mtwara


 Rais Jakaya Kikwete amekemea vikali vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara kusini mashariki mwa Tanzania baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Akizungumza mjini Dodoma, Rais Kikwete amesema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali. Aliongeza kuwa rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote. Akizungumza bungeni jana Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema mradi wa kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, umeanza kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda huko wiki ijayo kuweka jiwe la msingi. Tamko hili la Muhongo ndilo lililoibua vurugu kubwa Mtwara. Aidha jambo lingine linalosemekana limesababisha ghasia hizo ni hatua ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutokurusha moja kwa moja matangazo ya Bunge hivyo kuwakosesha wananchi fursa ya kusikiliza bajeti hiyo. Baadhi ya duru zinasema mtu mmoja amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kutokana na vurugu hizo. Milio ya risasi za moto na mabomu ya machozi vilisikika katika maeneo kadhaa ya Mtwara ambako hali ilikuwa mbaya kutokana na kuzuka mapambano kati ya polisi na vijana waliokuwa na hasira.
Posted by Unknown at 11:29:00 AM
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Newer Post Older Post Home
Powered By Blogger

My links

  • Singida connection facebook group
  • Singida connection
  • soundcloud

Vistors

Followers

About Me

Unknown
View my complete profile

BLOG ARCHIVES

  • June (1)
  • May (1)
  • September (20)
  • August (18)
  • July (2)
  • June (60)
  • May (42)
  • December (2)
  • October (6)
  • September (46)
  • August (116)
  • July (282)
  • June (92)

Blog zingine

Popular Posts

  • Wabunge watoro wakalia kuti kavu
    SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, ametangaza utaratibu mpya ambao utawabana vikali wabunge watoro wanaokwepa kuhudhuria vikao vya Bunge bila sab...
  • Dk. Slaa: CCM wachochezi
    KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa wamebaini mpango wa makusudi unaofanywa ...
  • CCM yapumulia mashine • Ajali ya mv Skagit, urais 2015 vyaitesa
    UPEPO wa mabadiliko ya kisiasa uliozikumba nchi nyingi duniani, unaelekea kukiathiri Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho sasa kinahaha kujinus...

Online

DFM. Powered by Blogger.