Friday, May 24, 2013

Hali bado tete Mtwara

Hali mkoani Mtwara, kusini ya Tanzania, inaendelea kuwa ya wasiwasi kufuatia ghasia za hapo majuzi kupinga uamuzi wa serikali kutaka kujenga bomba la kusafirisha gesi kutoka eneo hilo kuelekea Dar es Salaam.

Mapema, Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, aliliambia Bunge kwamba serikali imelazimika kutuma wanajeshi kutuliza hali, na sasa Waziri huyo anaripotiwa kuwapo Mtwara kutuliza hali juu ya kinachoendelea katika mkoa huo wa sasa.