Monday, July 23, 2012

Maiti zaidi wa MV. Skagit wapatikana



Naibu Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasilisno Zanzibar, Issa Haji Gavu,

Wakati zoezi la kutafuta meli iliyozama ya MV Skagit likiwa limesitishwa kutokana na uhaba wa vifaa, idadi ya maiti waliopatikana imeongezeka hadi kufikia 76 baada ya nyingine nane kuokotwa baharini Zanzibar.

Maiti hizo zilipatikana jana baada ya kukutwa wavuvi zikiwa zimeharibika kwenye maeneo ya Mwambao wa Bahari ya Hindi katika Kisiwa cha Chumbe maili sita kutoka ilipo Bandari ya Malindi Zanzibar.

Naibu Waziri wa Miundo Mbinu na Mawasilisno Zanzibar, Issa Haji Gavu, alithibitisha kupatikana kwa maiti hizo na kuzikwa katika Makaburi ya Kama visiwani hapa.

CHANZO: NIPASHE