Thursday, August 30, 2012

WAANDISHI WA HABARI SINGIDA WATAKIWA KUTOINGIZA USHABIKI KATIKA UTENDAJI WA KAZI.


Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Singida (Singpress) Seif Takaza akizungumza muda mfupi kabla hajamkaribisha mkuu wa wilaya ya Iramba kufungua mkutano maalum wa klabu hiyo kwa ajili ya kurekebisha katiba yao. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda.



Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Yahaya Nawanda akifungua mkutano maalum wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida kwa ajili ya kuifanyia marekebisho katiba yao. Wa kwanza kulia ni makamu mwenyekiti wa Singpress Jumbe Ismael na anayefuatia ni mwenyekiti wa Singpress Seif Takaza.

Baadhi ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano maalum wa klabu hiyo kufanya marekebisho ya katiba. Mkutano huo ulifanykia kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Iramba mjini New Kiomboi.




Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda (wa pili kulia – mwenye miwani) akiwa kwenye picha ya pamoja na wananchama wa Singpress.

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Yahaya Nawanda amewataka waandishi wa habari kuzingatia na kutii katiba zao kikamilifu, ili pamoja na mambo mengine, kuondoa uwezekano wa kutokea kwa migogoro inayohatarisha ustawi wa tasnia nyeti ya uandishi wa habari.


Nawanda ametoa wito huo wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa marekebisho ya katiba ya Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa SIngida (Singpress).

Amesema faida za kutii na kuzingatia katiba mahali popote pale, zipo nyingi ikiwemo ya kuimarisha amani na utulivu katika sehemu husika.

Aidha mkuu huyo wa wilaya amewasisitiza wahakikishe hawaendi tofauti na mabadiliko watakayoyafanya, baada ya marekebisho hayo, basi ni muhimu viongozi na wajumbe wote, mfuate kwa dhati na kuheshimu katiba yenu.

Akisisitiza zaidi, Nawanda amewataka waandishi hao wa habari, wasiingize ushabiki wa aina yo yote katika utendaji wao wa kazi za kila siku.

Nawanda amesema kazi ya uandishi wa habari sio kazi ambayo kila mtu anaweza kuifanya, ni lazima isomewe na mhusika awe na maadili.